Kanuni Mpya za Mfungaji Bora Ligi Kuu Ya NBC Tanzania: Katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo kwa sasa hujulikana kama ligi kuu ya NBC, mbio za ufungaji bora zimepamba moto huku nyota Stephanie Aziz Ki kutoka Klabu ya Yanga na Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ wa Azam FC wakiwa wanaongoza mbio hizi . Msimu uliopita, tulishuhudia mjadala mkali baada ya Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibazonkiza wa Simba kufikia idadi sawa ya mabao 17 kila mmoja, wakiwa wameongoza orodha ya ufungaji bora. Mwisho wa siku, wote wawili walipewa tuzo ya ufungaji bora, ukionyesha ushindani mkubwa katika ligi ya Tanzania.
Kanuni Mpya za Mfungaji Bora Ligi Kuu Ya NBC Tanzania
Katika msimu wa 2023/2024, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika jinsi mfungaji bora wa Ligi Kuu anavyopatikana. Hii ni baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufanya mapitio ya kanuni za kuamua mfungaji bora wa ligi. Hapa ndivyo taratibu za kumpata mfungaji bora wa Ligi Kuu kwa msimu wa 2023-24 zilivyo kikanuni:
Kanuni ya 11 (Vikombe na Tuzo)
13.1. Magoli yaliyofungwa kwa njia ya kawaida yatahesabiwa kuwa na alama mbili (2), na magoli yaliyofungwa kwa njia ya penalti yatahesabiwa kuwa na alama moja (1). Mchezaji mwenye alama nyingi atatangazwa kuwa mshindi.
13.2. Katika hali ya linganisho la alama, mchezaji aliyecheza muda mchache zaidi atapewa kipaumbele.
13.3. Iwapo wachezaji watapatana katika vigezo vyote viwili hapo juu, mchezaji aliyefunga mabao mengi ugenini atatangazwa kuwa mshindi.
13.4. Katika mashindano ya mtoano, mchezaji atakayekuwa katika timu iliyofika hatua ya juu zaidi ndiye atakayetajwa mshindi wa zawadi ya ufungaji bora. Iwapo hatua hii itashindwa kutambua mshindi, vipengele vya i-iii vitatumika kwa mpangilio wake.
Kwa mujibu wa kanuni hii, je, nyota wa timu yako atachukua kiatu cha ufungaji bora?
Machaguo ya Mhariri:
Weka Komenti