Kocha Ken Odhiambo Asema Bandari Imejipanga Kumkabili Bingwa Yanga

Kocha Ken Odhiambo Asema Bandari Imejipanga Kumkabili Bingwa Yanga

Kocha Mkuu wa Bandari FC, Ken Odhiambo, ameweka wazi kuwa kikosi chake kipo tayari kwa pambano dhidi ya mabingwa wa Tanzania, Yanga SC, akisisitiza maandalizi yao ni thabiti na yana lengo la kuonyesha ubora wao mbele ya mashabiki. Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuvuta hisia za wengi, Odhiambo alieleza kuwa anafahamu fika anakwenda kukutana na timu yenye heshima kubwa barani Afrika na wachezaji wa kiwango cha juu, lakini Bandari imejipanga kuhakikisha inatoa ushindani wa kweli.

“Yanga ni timu bora Afrika na ina wachezaji wengi wazuri. Huu mchezo tunauchukulia kwa ukubwa na tunatambua unatazamwa na mashabiki kutoka mataifa mbalimbali. Ni wakati mzuri kuonyesha ubora wetu,” alisema Odhiambo.

Kocha Ken Odhiambo Asema Bandari Imejipanga Kumkabili Bingwa Yanga

Maandalizi ya Bandari na Ushindani Unaotarajiwa

Kwa mujibu wa Odhiambo, Bandari itaingia uwanjani kwa heshima kubwa kwa Yanga lakini lengo kuu ni kuhakikisha wanatoa burudani na ushindani mkali. Aliwataka mashabiki kujiandaa kushuhudia mchezo wenye hadhi ya kimataifa, hasa ikizingatiwa utachezwa katika kilele cha Wiki ya Mwananchi, sherehe kubwa ya Yanga inayokusanya mashabiki wengi.

“Hautakuwa mchezo rahisi, lakini tumejiandaa vizuri. Mashabiki kutoka mataifa mbalimbali watarajie burudani ya kiwango cha juu,” aliongeza Odhiambo.

Kauli ya Nahodha Denis Nganga

Nahodha wa Bandari, Denis Nganga, naye alionyesha matumaini makubwa kuelekea mchezo huo. Akiwaongoza wenzake, alisisitiza kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha na wanajua wazi wanakutana na wachezaji hatari wa Yanga.

Nganga alimtaja wazi washambuliaji Clement Mzize na Andy Boyeli, akisema ni wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao Bandari italazimika kuwadhibiti kwa umakini.

“Tunatarajia kukutana na timu nzuri yenye wachezaji bora. Mzize na Boyeli ni washambuliaji hatari, wanahitaji kuchungwa kwa makini. Kikosi chetu kipo tayari na tunataka kutoa ushindani pamoja na burudani nzuri kwa mashabiki,” alisema nahodha huyo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Bakari Mwamnyeto Atoa Wito Kwa Mashabiki Kujitokeza Kwa Mkapa
  2. Mbosso Avunja Rekodi za Burudani Simba Day Kwa Performance Bora Zaidi
  3. Mbosso Avunja Rekodi za Burudani Simba Day Kwa Performance Bora Zaidi
  4. Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026
  5. Safari ya Ronaldo Kuelekea Mabao 1000 Yafikia Hatua Mpya Baada Kufunga Dhidi Hungary
  6. Azam FC Yawapa Mkono wa Kwaheri Wanne Kwa Mpigo
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo