Kylian Mbappé Atangaza Kuondoka PSG Huku Kukiwa na Tetesi za Kujiunga Real Madrid
- Baada ya kipindi cha miezi kadhaa kilichojaa uvumi na kutokuwa na uhakika, nyota wa soka wa Ufaransa, Kylian Mbappé, ametangaza siku ya Ijumaa kwamba anaondoka Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu wa Ligue 1 wa 2023-24.
Kylian Mbappé Atangaza Kuondoka PSG
Katika chapiso lake la video lililowekwa kwenye mitandao ya kijamii, Mbappé aliweka wazi kwamba hataongeza mkataba wake na mabingwa wa Ufaransa zaidi ya msimu huu na kwamba mchezo wake wa mwisho nyumbani akiwa na PSG utakuwa dhidi ya Toulouse Jumapili.
View this post on Instagram
Japo hakuna taarifa rasmi kuhusu kibarua chake baada ya PSG, uvumi wa uhamisho wa Mbappé kuelekea Real Madrid sio kitu kipya kwa masikio ya mashabiki wa mpira wa miguu na wengi wanaamini kua Real Madrid ndio klabu yenye nafasi kubwa kudaka saini ya Mbappe baada ya kuanza kuiwinda tangu msimu uliopita wa joto.
Mnamo Februari, ripoti kutoka kwa mtangazaji wa BBC Sport, Guillem Balague, iliripoti kwamba licha ya kutokuwa na mkataba rasmi na Real Madrid wakati huo, Mbappé alikuwa amekubali mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo, ambao ungekuwa na malipo ya Euro milioni 15 (takriban dola milioni 16) kwa msimu na bonasi ya Euro milioni 150 (sawa na dola milioni 161) kusaini mkataba.
Mbappé, mwenye umri wa miaka 25, ameshiriki kwa misimu saba na PSG tangu ajiunge nao kutoka AS Monaco msimu wa 2017-18.
Katika msimu huu, Mbappé amefunga jumla ya mabao 26 katika mechi 28 za Ligue 1, huku akiendelea kuonyesha umahiri wake katika uwanja wa mpira kwa msimu wa nne mfululizo akiwa na wastani wa mabao kati ya 26 na 29 kwa kila msimu wa ligi.
Vilevile, amefunga jumla ya mabao 43 katika mechi 46 za mashindano yote msimu huu, akithibitisha ubora wake na kushikiria rekodi yake ya kufunga zaidi ya magoli 40 kwa misimu mitatu katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Ikiwa na uongozi wa Mbappé katika safu ya ushambukliaji, PSG wameshikilia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligue 1 wakiwa na jumla ya pointi 70 msimu huu, wakiwaacha nyuma kwa pointi tisa timu ya pili, Monaco.
Klabu hiyo tayari imetwaa taji lao la sita la Ligue 1 chini ya uongozi wa Mbappé, na pia wakimaliza kama washindi wa pili katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA mnamo 2020.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Makocha wanaowania Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka 2023/2024 Ligi Kuu ya Uingereza
- Orodha ya Wachezaji Wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana EPL 2023/2024
- Fainali Ya Klabu Bingwa Afrika 2024: Timu, Tarehe, Na Mahali
- Cheki Picha: Jezi Mpya za Liverpool kwa Msimu wa 2024/2025
- Fainali ya UEFA Champions League 2024: Real Madrid vs. Borussia Dortmund
- Kanuni Mpya za Mfungaji Bora Ligi Kuu Ya NBC Tanzania 2023/2024
Weka Komenti