Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam jimbo la Ukonga

Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam jimbo la Ukonga

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Jimbo la Ukonga imetangaza rasmi orodha ya majina ya waombaji waliochaguliwa kufanya usaili wa kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025. Tangazo hili muhimu limetolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ukonga, likiwa ni utekelezaji wa masharti ya kifungu cha 6(6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, sambamba na Kanuni ya 11 ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwaka 2025.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, usaili huo unalenga kuhakikisha uteuzi wa wasimamizi wenye sifa, weledi, na uadilifu watakaosaidia katika kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 unafanyika kwa uwazi, haki, na ufanisi mkubwa.

Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam jimbo la Ukonga

Tarehe na Mahali pa Kufanyika kwa Usaili

Waombaji wote waliochaguliwa kuudhulia kwenye usaili wanapaswa kufika kwa ajili ya usaili siku ya Jumatano, tarehe 15 Oktoba 2025, katika Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo Gongolamboto, kuanzia saa 2:00 asubuhi. Ni muhimu kuzingatia muda huu kwani usaili utaanza kwa wakati uliopangwa bila kuchelewa.

Maelekezo Muhimu kwa Washiriki

Wote walioitwa kwenye usaili huu wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

  • Usaili utaanza saa 2:00 asubuhi – hakikisha umefika mapema ili kuepuka kukosa fursa.
  • Msailliwa atagharamia mwenyewe gharama zote za usafiri, chakula na malazi wakati wa zoezi hili.
  • Fika na kitambulisho halali, iwe ni barua ya utambulisho kutoka ofisi ya Serikali za Mitaa au kitambulisho kingine kinachotambulika rasmi.

Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Jimbo la Ukonga Pdf

Orodha kamili ya majina ya waombaji waliochaguliwa kufanyiwa usaili kwa ajili ya nafasi za kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Jimbo la Ukonga imetolewa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ukonga.

Majina haya yanahusisha waombaji walioteuliwa kushiriki katika usaili kwa nafasi za:

  1. Msimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura,
  2. Msimamizi Msaidizi wa Kituo, na
  3. Karani Mwongoza Wapiga Kura.

Kwa mujibu wa tangazo rasmi, waombaji wote waliotajwa wanapaswa kufika kwenye usaili tarehe 15 Oktoba 2025, Chuo Kikuu cha Kampala – Gongolamboto, kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Bofya Hapa Kupakua Tangazo Rasmi la Usaili jimbo la Ukonga

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Segerea
  2. Majina Ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Jimbo La Lupembe
  3. Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Jimbo la Ilala
  4. Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Manispaa Ya Kinondoni
  5. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili INEC 2025
  6. Posho na Malipo ya Wasimamizi wa Uchaguzi 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo