Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Segerea

Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Segerea

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Segerea imetoa tangazo rasmi lenye orodha ya waombaji waliopangwa kushiriki kwenye usaili wa nafasi za Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura na Wasimamizi Wasaidizi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Tangazo hili limebainisha utaratibu na tarehe maalum ya usaili, ikiwa ni hatua muhimu katika maandalizi ya uchaguzi huo mkuu wa kitaifa. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, usaili utafanyika tarehe 15 Oktoba 2025, katika Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo Gongolamboto, kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Segerea amesisitiza umuhimu wa washiriki kufika kwa wakati na kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa ili kufanikisha mchakato huu muhimu.

Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Segerea

Maelekezo Muhimu kwa Washiriki wa Usaili

Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wote waliotajwa kwenye orodha rasmi wanatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo wakati wa kufika kwenye eneo la usaili:

  • Muda wa kuanza usaili: Saa 2:00 asubuhi bila kuchelewa.
  • Gharama za usaili: Kila msailiwa atagharamia usafiri, chakula na malazi binafsi.
  • Vitambulisho: Washiriki wanapaswa kufika wakiwa na kitambulisho cha Taifa (NIDA), leseni, au barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali za Mitaa.
  • Nidhamu na maandalizi: Washiriki wanahimizwa kuvaa kwa heshima na kufuata taratibu zote za eneo la usaili.

Orodha ya Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Segerea

Halmashauri imetoa orodha ndefu ya majina ya waombaji waliopitishwa kushiriki katika hatua ya usaili. Orodha hiyo inajumuisha mamia ya majina kutoka maeneo mbalimbali ya Jimbo la Segerea, wakiwemo vijana, watumishi wa umma na raia wenye sifa stahiki waliowasilisha maombi yao kwa nafasi hizo.

Baadhi ya majina yaliyotajwa katika orodha rasmi ni kama ifuatavyo:

  • ABDIYYA M. ALLY
  • ALIZABETH PETER
  • AMINA SHABANI MOHAMEDY
  • ANTONY ALFRED MKINGA
  • BEATRICE CHARLES GABONE
  • GLORY DISMAS MAEMBE
  • HADIJA H. NKUSA
  • IRENE MWAMBOLA
  • MARYSALOME JUSTIN LAMOSAI
  • NEEMA ISACK MOLLEL
  • SIGFRIDI JOACHIM OMARI
  • VERONICA ERNEST SAMA, na wengine wengi.

Orodha kamili ya majina yote yaliyopitishwa imeambatanishwa katika kiungo kilichopo hapa chini ambapo kitakuwezesha kupakua tangazo rasmi lililotolewa na ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Segerea.

Bofya Hapa Kupakua Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Segerea Pdf

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Manispaa Ya Kinondoni
  2. Posho na Malipo ya Wasimamizi wa Uchaguzi 2025
  3. Nafasi za Kazi Ualimu 2025: Serikali Yatangaza Ajira Mpya 12,176 kwa Walimu
  4. Serikali Yatangaza Ajira Mpya za Afya October 2025
  5. Nafasi Mpya za Kazi Serikalini 2025/2026 – Sekta ya Elimu, Afya, na Ulinzi Zapewa Kipaumbele
  6. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili INEC 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo