Majina ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja 2024/2025

Majina ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja 2024/2025 | Orodha ya Waombaji waliodahiliwa zaidi ya Chuo Kimoja au Programu zaidi ya moja mwaka wa masomo 2024/2025

Katika mwaka wa masomo 2024/2025, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu zaidi ya kimoja. Hatua hii imekuja baada ya kumalizika kwa dirisha la kwanza la maombi ya udahili, ambapo idadi kubwa ya waombaji walifanikiwa kupata nafasi za masomo katika vyuo mbalimbali nchini. Kwa wale ambao wamechaguliwa kujiunga na zaidi ya chuo kimoja, wanatakiwa kufanya uthibitisho wa chuo kimojawapo ili kuhakikisha nafasi yao inahifadhiwa.

Uthibitisho wa Udahili: Jinsi ya Kufanya

Wanafunzi waliochaguliwa katika vyuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao kwa kutumia namba maalum ya siri (PIN) iliyotumwa kupitia ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu zao au barua pepe walizotumia wakati wa maombi. Uthibitisho huu unapaswa kufanyika kati ya tarehe 4 Septemba na 21 Septemba, 2024.

Hatua za Kuthibitisha Udahili

  • Kupokea Namba ya Siri: Hakikisha umepokea namba ya siri kupitia SMS au barua pepe. Iwapo hujapokea ujumbe huo, ingia kwenye mfumo wa udahili wa chuo husika na omba kutumiwa upya.
  • Ingia Kwenye Akaunti Yako ya Udahili: Tembelea tovuti ya chuo ulipochaguliwa na ingia kwenye akaunti yako ya udahili.
  • Weka Namba ya Siri: Tumia namba hiyo kuthibitisha udahili wako kwenye chuo kimojawapo.
  • Thibitisha Chuo Kimojawapo: Baada ya kuweka namba ya siri, chagua chuo unachotaka kujiunga nacho na thibitisha chaguo lako.
    Umuhimu wa Kuthibitisha Mapema:
  • Ni muhimu kuthibitisha udahili wako mapema ili kuepuka kupoteza nafasi yako ya masomo. Wale ambao hawatathibitisha udahili wao ndani ya muda uliopangwa, watapoteza nafasi yao, na vyuo vinaweza kuwasajili wanafunzi wengine kwenye nafasi hizo.

Majina ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja 2024/2025

TCU imeweka orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja kwenye tovuti yao rasmi. Wanafunzi wanashauriwa kuangalia orodha hii ili kujua kama wako miongoni mwa waliochaguliwa. Pia Hapa Habariforum tumekuletea pdf rasmi yenye Orodha ya Waombaji wote waliodahiliwa zaidi ya Chuo Kimoja au Programu zaidi ya moja mwaka wa masomo 2024/2025.

Majina ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja 2024/2025
Majina ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja 2024/2025

Bofya Hapa Kupakua Majina ya Waliochaguliwa Chuo zaidi ya Kimoja

NEW Bofya Hapa Kupakua Majina ya Waliochaguliwa Chuo zaidi ya Kimoja Awamu ya Pili

Dirisha la Pili la Maombi ya Udahili

Kwa wale ambao hawakupata nafasi au walikosa kufanya maombi kwenye dirisha la kwanza, TCU imefungua dirisha la pili la maombi kuanzia tarehe 3 Septemba hadi 21 Septemba, 2024. Hii ni fursa nyingine kwa wanafunzi kuhakikisha wanapata nafasi ya kujiunga na programu za shahada za awali kwenye vyuo vikuu nchini. Wanafunzi wanashauriwa kuwa makini katika kuchagua programu za masomo na kuhakikisha wanazingatia viwango vya udahili vinavyotakiwa na chuo husika. Aidha, ni muhimu kuhakikisha kwamba vyuo walivyochagua vinakidhi matarajio yao ya kitaaluma na malengo ya baadaye.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Waliochaguliwa kujiunga na vyuo Vikuu 2024/2025
  2. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo 2024
  3. Waliochaguliwa kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa 2024/2025
  4. Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha Ardhi (ARU) 2024/2025
  5. Majina ya Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo