Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Jeshi la Polisi 2025
Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza rasmi majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi hilo kwa mwaka 2025. Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, vijana hao wametakiwa kuripoti katika Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 12 Juni 2025 hadi 14 Juni 2025 kwa ajili ya kuanza rasmi mafunzo yao. Tangazo hili limekuja baada ya kukamilika kwa mchakato wa usaili uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani, ambapo vijana waliopitia hatua hizo sasa wametakiwa kuanza maandalizi ya kujiunga rasmi na Jeshi la Polisi la Tanzania.
Taarifa Muhimu kwa Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2025
📍 Tarehe za Kuripoti Shule ya Polisi Moshi
Vijana wote waliopata nafasi wanapaswa kuhakikisha kuwa wanaripoti kati ya tarehe 12/06/2025 hadi 14/06/2025. Muda wa kuripoti ni muhimu, kwani yeyote atakayefika baada ya tarehe 14 Juni hatapokelewa na atachukuliwa kuwa amejiuzulu kwa hiari yake.
🚌 Maandalizi ya Safari kwa Makundi Mbali Mbali
- Waliofanyiwa usaili Dar es Salaam: Wanatakiwa kuripoti tarehe 12 Juni 2025, saa 12:00 asubuhi, katika uwanja wa gwaride wa Police Barracks uliopo barabara ya Kilwa (nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road) kwa ajili ya kusafiri kuelekea Moshi.
- Waliofanyiwa usaili Mikoa mingine ya Tanzania Bara: Wataripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa husika tarehe 11 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi ili kupewa utaratibu wa kusafiri.
- Waliofanyiwa usaili Zanzibar (Unguja na Pemba): Wataripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya safari.
Vifaa Muhimu kwa Mafunzo ya Polisi
Vijana wote wanaopaswa kuripoti Shule ya Polisi Moshi wanatakiwa kwenda wakiwa na vifaa vifuatavyo:
👕 Mavazi ya Mazoezi na Malazi
- Traki suti ya rangi ya bluu yenye ufito mweupe
- Fulana nyeupe isiyo na maandishi
- Raba na soksi nyeusi
- Bukta mbili za bluu (kwa ajili ya michezo na mazoezi)
- Sanduku la chuma (tranka) la rangi ya bluu
- Chandarua cheupe cha duara (sio pembe nne)
- Shuka za rangi ya bluu mpauko jozi mbili (shuka 4)
- Blanketi moja la kijivu lisilo na maua (sio duveti)
- Pasi ya mkaa
🍽️ Vifaa vya Kutumia na Usafi Binafsi
- Kikombe cha plastiki cha rangi ya cream light (material ya mfupa)
- Sahani aina ya steel dish plate
- Vifaa vya usafi: sururu moja yenye mpini, ndoo mbili ndogo, fagio la chelewa
📑 Nyaraka Muhimu
- Vyeti halisi vya taaluma
- Cheti halisi cha kuzaliwa
- Kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA)
- Nakala za kadi au namba za NIDA za wazazi na ndugu wa karibu (Baba, Mama, Mjomba, nk)
- Picha ndogo (passport size) 6 zenye mandharinyuma ya bluu
- Nakala 5 za kila cheti kilichoainishwa
💰 Mahitaji ya Ziada
- Kadi ya Bima ya Afya (NHIF) kama anayo au fedha taslimu Tsh. 50,400/= kwa wasio nayo
- Fedha za kujikimu kwa matumizi binafsi
⚠️ Tahadhari Muhimu Kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga Mafunzo ya Polisi
Simu za mkononi haziruhusiwi kabisa Shule ya Polisi Moshi. Mwanafunzi atakayepatikana na simu atachukuliwa kuwa ameonyesha utovu wa nidhamu na atafukuzwa mara moja.
Utaratibu wa kuwasiliana na familia utatolewa na shule baada ya kuripoti.
Kwa vijana wote waliochaguliwa, kutofika kwa wakati ni sawa na kujiondoa rasmi katika nafasi hiyo.
📃 Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa
Orodha kamili ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa kwenye tangazo rasmi la Jeshi la Polisi na pia tumekuletea hapa chini ili kurahisisha zoezi zima la upatikanaji wa orodha hio. Wanaotaka kuangalia majina yao wanashauriwa kufuatilia kupitia tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi Tanzania, ofisi za polisi za mikoa au matangazo ya serikali.
TANGAZO_LA_KURIPOTI_SHULE_YA_POLISI_MOSHIMapendekezo ya Mhariri:
- Vitu vya Kwenda Navyo JKT Mujibu Wa Sheria 2025
- Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)
- Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2025/2026
- Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 Mujibu wa Sheria
- Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026
- Tarehe ya Kuripoti Makambini JKT Mujibu wa Sheria 2025
- Ni Lini TAMISEMI Itatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026?
Leave a Reply