Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Magereza 2025

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Magereza 2025

Jeshi la Magereza nchini limetangaza orodha rasmi ya waombaji wa ajira waliofanikiwa kuingia kwenye hatua ya usaili kwa mwaka 2025, baada ya kufanya uchambuzi wa maombi yaliyowasilishwa kupitia mfumo wa Tanzania Prisons Service Recruitment Management System (TPSRMS). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza, usaili huo utafanyika kuanzia 17–23 Novemba 2025 katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, huku kwa ngazi ya mikoa ukitekelezwa tarehe 17 Novemba 2025, kuanzia saa 02:00 asubuhi.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa gharama za chakula, usafiri na malazi zitaendelea kubebwa na wahusika wenyewe, sambamba na wajibu wa kufika kwenye usaili wakiwa na vyeti halisi vya elimu, cheti cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma (kwa walioomba kada maalum), pamoja na kitambulisho cha NIDA. Kamishna Jenerali amesisitiza kuwa utekelezaji wa hatua hii unalenga kuhakikisha mchakato wa ajira unazingatia “vigezo vya awali vilivyoainishwa” kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Magereza.

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Magereza 2025

Nyaraka Zinazotakiwa Kwa Ajili ya Usaili

Kwa mujibu wa tangazo, waombaji wote walioitwa wanapaswa kufika kwenye usaili wakiwa na nyaraka zifuatazo:

  1. Cheti halisi cha Elimu ya Sekondari
  2. Cheti halisi cha kuzaliwa
  3. Cheti halisi cha Taaluma (kwa walioomba nafasi za fani maalumu)
  4. Kitambulisho cha Taifa (NIDA)

Jeshi la Magereza limekazia kuwa wahusika wote wanapaswa kufika na nyaraka halisi, sio nakala.

Orodha Kamili ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Magereza 2025

Kama wewe ni miongoni mwa maelfu ya waliotuma maombi ya kazi jeshi la magereza na ungependa kujua kama umechaguliwa kushiriki hatua ya usaili basi hapa chini tumekuletea pdf yenye majina yote na taarifa kuhusu zoezi zima la usaili wa jeshi la magereza november 2025. Orodha ya walioitwa kwenye usaili imepangiliwa kwa kuzingatia mkoa wa kufanyia usaili, kama ilivyoainishwa kwenye PDF ya Jeshi la Magereza.

majina magereza

Bofya Hapa Kupakua Pdf

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025
  2. Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Kusimamia Uchaguzi 2025 Dodoma
  3. Nafasi Mpya 10026 za Kazi Walimu MDAs & LGAs 2025
  4. Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal
  5. Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025
  6. Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo ya Kusimamia Uchaguzi INEC 2025 Mkoa wa Singida
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo