Matokeo Afrika Kusini vs Taifa Stars Leo 06/06/2025 | Matokeo ya Mechi ya Kirafiki Taifa Stars vs Afrika Kusini
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania, almaarufu kama Taifa Stars, leo Ijumaa tarehe 06 Juni 2025 itashuka dimbani katika dimba la Peter Mokaba lililopo mjini Polokwane, Afrika Kusini kumenyana na wenyeji wao Bafana Bafana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki. Mchezo huu unatarajiwa kuanza saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (saa 1:30 kwa saa za Afrika Kusini), huku ukiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kwa pande zote mbili kuelekea mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Kikosi cha Taifa Stars tayari kimewasili salama nchini Afrika Kusini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo, Johannesburg saa 2:00 asubuhi kwa saa za huko (saa 3:00 kwa saa za Tanzania).
Hata hivyo, kikosi hicho hakikuambatana na wachezaji wawili muhimu – beki Shomari Kapombe wa Simba SC ambaye ni mgonjwa, na winga machachari Suleiman Mwalimu ‘Gomez’ wa Wydad AC ya Morocco ambaye alitarajiwa kuwasili baadaye leo. Nahodha wa Taifa Stars, Mohamed Hussein maarufu kama Tshabalala, ameweka wazi kuwa lengo la timu ni kupata ushindi dhidi ya Bafana Bafana. “Tuna kikosi imara na morali ya hali ya juu. Tunaamini tunaweza kupata matokeo chanya dhidi ya Afrika Kusini,” alisema kwa kujiamini.
Matokeo Afrika Kusini vs Taifa Stars Leo 06/06/2025
Afrika Kusini | VS | Tanzania |
Bafana Bafana Wakabidhiwa Jukumu la Kuwakilisha Bila Mastaa wa Mamelodi Sundowns
Bafana Bafana wamekuwa kambini Johannesburg tangu Juni 1, wakijifua kwa ajili ya mchezo huu. Kikosi cha awali kilichoitwa na kocha wao Hugo Broos kilikuwa na jumla ya wachezaji 41, ingawa kitaratibiwa na kupunguzwa hadi wachezaji 23 pekee kabla ya mchezo.
Ni muhimu kueleza kuwa hakuna mchezaji yeyote kutoka klabu ya Mamelodi Sundowns aliyeitwa katika kikosi hicho kutokana na klabu hiyo kuwa na maandalizi ya kushiriki Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika Marekani kuanzia Juni 14 hadi Julai 13, 2025.
Bafana Bafana wamejumuisha wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika Kusini kupitia Ligi Kuu ya PSL, wakichanganywa na wachache wanaocheza nje ya nchi kama vile:
- Mihlali Mayambela – Aris Limassol (Cyprus)
- Siyabonga Ngezana – FCSB
- Samukelo Kabini – Molde
- Luke le Roux – Varnamo
- Bongokuhle Hlongwane – FC Minnesota
- Shandre Campbell – Club Brugge
Kikosi cha Bafana Bafana kinajumuisha vipaji mchanganyiko kutoka klabu mbalimbali kama vile Orlando Pirates, Kaizer Chiefs, Supersport United, Stellenbosch, TS Galaxy, Sekhukhune United, Richards Bay, Polokwane City na Amazulu. Hii inaonesha dhamira ya kutumia mchezo huu kama jukwaa la kupima wachezaji wapya na kuimarisha kikosi kuelekea michuano ya baadaye.
Taifa Stars Waelekea COSAFA Mechi ya Leo Dhidi Afrika Kusini ni Kipimo Muhimu
Mara baada ya mchezo huu wa kirafiki, Taifa Stars wanatarajiwa kuelekea mjini Bloemfontein ili kushiriki Mashindano ya COSAFA Cup yanayoanza kesho Juni 7, 2025. Tanzania imepangwa Kundi C pamoja na Madagascar na Eswatini. Mechi yao ya kwanza itakuwa dhidi ya Madagascar, ikifuatiwa na ile dhidi ya Eswatini Juni 11.
Mkuu wa msafara wa Taifa Stars, James Mhagama, ameeleza kuwa mchezo wa leo ni sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha kikosi kinaanza kwa kishindo katika mashindano hayo. “Tumejipanga vizuri, tupo Afrika Kusini sio kwa matembezi, bali kwa kuhakikisha tunalinda heshima ya Taifa letu katika COSAFA,” alisisitiza Mhagama.
Historia ya Taifa Stars katika COSAFA – Je, Mwaka Huu Watafanya Vyema Zaidi?
Mwaka 2017, Taifa Stars walishiriki michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini na kufika hatua ya Nusu Fainali, ambako walitolewa na Zambia kwa mabao 4-2. Katika mashindano hayo, Tanzania iliifunga Malawi 2-0, na kutoa sare dhidi ya Mauritius (1-1) na Angola (0-0), kabla ya kuwatoa wenyeji Afrika Kusini kwa bao 1-0 lililofungwa na Elias Maguri.
Kwa msingi huo, mchezo wa leo dhidi ya Bafana Bafana unachukuliwa kama kipimo tosha cha uwezo wa kikosi cha Kimataifa cha Tanzania kuelekea kuandika historia mpya katika Kombe la COSAFA 2025.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Herry Sasii Afungiwa Soka Miezi 6 Kisa Mechi ya Simba na Singida
- Seif Karihe Acharazwa Faini na Kufungiwa Michezo Mitatu kwa Kurusha Chupa
- Ronaldo Aipeleka Ureno Fainali UEFA Nations League 2024/2025
- Matokeo ya Germany Vs Portugal Leo 04/06/2025
- Wachezaji wa Soka U-21 Waliofanya Vizuri Msimu wa 2024/2025
- Mabekio Waliochangia Magoli Mengi Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
- Siku ya Kuripoti Chuo cha Polisi Moshi 2025 kwa Vijana Waliochaguliwa
- Michezo ya Yanga Sc Iliobaki Msimu wa 2024/2025
- Wachezaji wa Yanga Walioitwa Kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa June 2025
Leave a Reply