Matokeo JKT Tanzania Vs Azam Leo 28/08/2024

Matokeo JKT Tanzania Vs Azam Leo 28/08/2024 | Matokeo ya Azam Leo Dhidi ya JKT Tanzania Ligi Kuu

Wana rambaramba Azam FC leo watakuwa katika kibarua cha Ligi Kuu ya NBC Tanzania ambapo watakalibishwa na JKT Tanzania katika mchezo wa kukatana shoka utakaotimua vumbi kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo majira ya saa 10 jioni. Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kusisimua, kwani ni mchezo wa kwanza wa msimu mpya wa ligi kwa timu zote mbili.

Baada ya kutupwa nje ya michuano ya kimataifa na APR ya Rwanda, Azam FC wapo kwenye harakati za kurejesha hadhi yao. Msimu uliopita, Azam ilifanikiwa kuvuna pointi sita dhidi ya JKT Tanzania katika mechi mbili zilizopita za ligi. Mchezo wa kwanza ulifanyika Desemba 11, 2023, ambapo Azam walishinda 2-1, na kisha wakarudia ushindi wa 2-0 mnamo Mei 21, 2024.

Hata hivyo, msimu huu mambo yanatarajiwa kuwa tofauti. Timu zote zimeimarisha vikosi vyao katika dirisha kubwa la usajili, na wachezaji wapya wanatarajiwa kuleta changamoto mpya. Azam FC, ambayo ilishika nafasi ya pili nyuma ya Yanga msimu uliopita, inatarajiwa kutumia uzoefu wao na nyota wapya kufanikisha ushindi katika mechi hii muhimu.

Kwa upande wa JKT Tanzania, timu hii inatarajia kuonyesha uwezo wao dhidi ya moja ya timu bora nchini. Wakiwa na nyota wao wa zamani wa Azam, John Bocco, wana matumaini ya kuanza msimu kwa ushindi. Bocco atakuwa na jukumu kubwa la kuongoza safu ya ushambuliaji ya maafande hao.

Kocha wa Azam FC, Youssouph Dabo, anaamini kuwa kikosi chake kitaendelea kutoka pale walipoishia msimu uliopita licha ya changamoto zilizowakumba katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Dabo anaeleza kuwa sasa wanajikita kwenye ligi na mashindano mengine ya ndani huku wakilenga kuanza msimu kwa ushindi.

Kwa upande wa kocha wa JKT Tanzania, Hamady Ally, anafahamu ukubwa wa changamoto inayowakabili, lakini ana matumaini makubwa kuwa timu yake itaweza kufanikisha ushindi. Maandalizi yote yamekamilika, na lengo kuu ni kuhakikisha wanapata mwanzo mzuri wa ligi.

Matokeo JKT Tanzania Vs Azam Leo 28/08/2024

JKT Tanzania 0-0 FTAzam Fc
  • 🚨 Mchezo🚨
  • JKT Tanzania🆚Azam Fc
  • 🏆 NBC Premier League
  • 🗓️ Round 1
  • 🏟 Meja Isamuhyo Stadium
  • 🕰 4.00 PM (E.A.T)

Matokeo JKT Tanzania Vs Azam Leo 28/08/2024

Rekodi za Timu Hizi

Rekodi za mechi zilizopita zinaonyesha kuwa Azam FC ina rekodi nzuri dhidi ya JKT Tanzania. Katika misimu minne iliyopita, Azam haijawahi kupoteza dhidi ya maafande hao. Wameshinda mechi sita, ikiwemo ushindi wa mabao 6-1 mnamo Machi 8, 2019, na wametoka sare mara mbili. Rekodi hii inawapa Azam FC morali wa kuendeleza ubabe wao katika mchezo huu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kengold Fc Vs Singida Black Stars Leo 18/08/2024 | Matokeo & Vikosi
  2. Kikosi cha Simba Vs Tabora United Leo 18/08/2024
  3. Matokeo ya Mashujaa Vs Dodoma Jiji Leo 17/08/2024
  4. Matokeo ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons Leo 16/08/2024
  5. Viingilio Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024
  6. Vikosi Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo