Matokeo ya Azam VS Simba Leo 08/01/2026
Wana rambaramba wa Azam FC leo wanakutana na Simba SC katika pambano kubwa la nusu fainali ya NMB Mapinduzi Cup 2026, mchezo unaotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka nchini kutokana na historia, ubora wa vikosi na kisasi kilichopo kati ya timu hizi mbili. Mechi hii ya dabi ya Mzizima inapigwa leo tarehe 08 Januari 2026, kuanzia saa 2:15 usiku katika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, huku macho na masikio ya mashabiki yakielekezwa kusubiri matokeo ya Azam VS Simba leo 08/01/2026.
Taarifa Muhimu za Mchezo
- Mashindano: NMB Mapinduzi Cup 2026
- Hatua: Nusu Fainali
- Uwanja: New Amaan Complex, Unguja
- Muda: Saa 2:15 usiku
- Matangazo ya Moja kwa Moja: Azam Sports 3 HD
Viingilio
- Orbit & Saa – 3,000/=
- Urusi – 5,000/=
- VIP – 10,000/=
Historia Fupi ya Dabi Hii
Ni takribani mwezi mmoja tu umepita tangu Azam FC na Simba SC zilipokutana katika Ligi Kuu ya NBC Bara, ambapo Azam iliondoka na ushindi wa mabao 2-0. Leo, dabi hiyo inarejea tena lakini safari hii ikiwa na uzito mkubwa zaidi kwa kuwa ni ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026. Ushindi hapa unamaanisha tiketi ya kwenda fainali, huku kipigo kikimaanisha kuishia njiani.
Kwa ujumla, nusu fainali zote za Mapinduzi Cup 2026 zimejaa harufu ya kisasi, ambapo Simba inatafuta kulipiza kisasi dhidi ya Azam, huku Azam ikisaka kuendeleza ubabe wake wa kihistoria kwenye michuano hiyo.
Safari ya Azam FC Hadi Nusu Fainali
Azam FC ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya kuongoza Kundi A kwa pointi saba. Kikosi hicho kilionyesha uimara mkubwa katika hatua ya makundi kwa:
- Ushindi wa 2-0 dhidi ya Mlandege
- Ushindi wa 2-1 dhidi ya URA
- Sare ya 1-1 dhidi ya Singida Black Stars
Matokeo hayo yaliipa Azam nafasi ya kuingia nusu fainali ikiwa na morali kubwa na matumaini ya kufika fainali.
Safari ya Simba SC Kufikia Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi
Simba SC, kwa upande wake, ilimaliza kinara wa Kundi B baada ya kushinda mechi zote mbili ilizocheza:
- Ushindi wa 1-0 dhidi ya Muembe Makumbi City
- Ushindi wa 2-1 dhidi ya Fufuni
Ushindi wa asilimia mia moja kwenye makundi unaifanya Simba iingie kwenye nusu fainali ikiwa na kujiamini, licha ya kumbukumbu ya kipigo cha hivi karibuni dhidi ya Azam kwenye ligi.
Hali ya Vikosi na Wachezaji Muhimu
Simba SC inatarajiwa kuimarika zaidi baada ya kurejea kwa mabeki Rushine De Reuck na Chamou Karaboue, ambao walipumzishwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Fufuni. Aidha, kurejea kwa Jean Charles Ahoua na Jonathan Sowah, waliokosekana kwenye mechi za makundi, kunaongeza nguvu mpya kikosini. Elie Mpanzu tayari ameshacheza mchezo mmoja uliosaidia Simba kufika nusu fainali.
Kwa upande wa Azam FC, kikosi kipo imara licha ya kukosa baadhi ya wachezaji walioko na timu ya taifa. Jephte Kitambala anaongoza safu ya ushambuliaji akiwa miongoni mwa vinara wa mabao baada ya kufunga mawili.
Ingawa Idd Nado anakosekana leo, Nassor Saadun, aliyekuwa mhusika muhimu kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba kwenye ligi, yupo kikosini licha ya kutocheza mechi za Mapinduzi Cup hadi sasa.
Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo
Kocha wa Simba SC, Steve Barker, ameutaja mchezo huu kama kipimo muhimu katika mchakato wa kuijenga timu:
“Nafahamu tulipoteza mechi msimu huu dhidi ya Azam. Kukutana na timu kubwa kama hii kipindi hiki kunanipa motisha ya kujua tupo wapi katika maandalizi yetu. Ili tufanye vizuri lazima tucheze kwa kasi na mbinu sahihi.”
Kwa upande wa Azam FC, kocha Florent Ibenge amesisitiza maandalizi na malengo ya timu:
“Kila mechi ina changamoto yake. Hatua ya makundi tulikutana na timu ngumu, sasa tunakwenda hatua ngumu zaidi. Tupo tayari kushindana na malengo yetu ni ubingwa na kujiimarisha kuelekea michezo ya CAF.”
Matokeo ya Azam VS Simba Leo 08/01/2026
| Azam Fc | 1-0 FT | Simba Sc |
- Lameck Lawi Anaitanguliza Azam Fc dakika ya 74 ya mchezo. Azam 1 Simba Sc 0
- Mpira Umemalizika Azam Fc imeshinda kwa goli 1-0 na itasonga mbele kucheza fainali dhidi mshindi wa mchezo wa kesho kati ya Yanga Sc vs Singida Black Star
Rekodi za Azam VS Simba Kwenye Mapinduzi Cup
Tangu Azam FC ilipoanza kushiriki Kombe la Mapinduzi mwaka 2011, timu hizi zimekutana mara saba katika michuano hiyo. Takwimu zinaonyesha:
- Azam FC imeshinda mechi tano
- Simba SC imeshinda mechi mbili
- Matokeo ya mikutano hiyo ni pamoja na:
- Azam 2-0 Simba (Nusu fainali 2012)
- Azam 2-2 Simba, Azam kushinda penalti 5-4 (Nusu fainali 2013)
- Azam 1-0 Simba (Fainali 2017)
- Azam 1-0 Simba (Makundi 2018)
- Azam 2-1 Simba (Fainali 2019)
- Azam 0-0 Simba, Simba kushinda penalti 3-2 (Nusu fainali 2020)
- Azam 0-1 Simba (Fainali 2022)
Rekodi hizi zinaongeza mvuto wa kusubiri kwa hamu matokeo ya Azam VS Simba leo 08/01/2026.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply