Yanga Vs KMC Leo 29/09/2024 Saa Ngapi?
Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) inazidi kushika kasi, na leo tarehe 29 Septemba 2024, mashabiki wa soka watashuhudia mechi kubwa kati ya watetezi wa ubingwa, Yanga SC, na timu ya Kinondoni Municipal Council (KMC). Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:00 usiku.
Fuatilia Hapa Matokeo ya Yanga Vs KMC Leo 29 September 2024
Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa imetoka kushinda michezo yake miwili ya hivi karibuni ya Ligi Kuu. Walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar na ushindi wa 1-0 dhidi ya KenGold. Hadi sasa, safu ya ulinzi ya Yanga imekuwa imara, ikiruhusu bao moja tu katika mechi nane walizocheza msimu huu kwenye mashindano mbalimbali, huku wakifunga jumla ya mabao 25.
Kwa upande wa KMC, wao hawajaanza msimu huu vizuri. Wameshinda mechi moja pekee, kupata sare moja na kupoteza michezo mitatu, wakifunga mabao matatu na kuruhusu mabao saba. Mshambuliaji wao tegemeo, Redemptus Musa, ameifungia timu hiyo mabao mawili kati ya mabao matatu waliyofunga kwenye ligi mpaka sasa. Hii inaonyesha namna KMC wanavyomtegemea mchezaji huyu katika safu ya ushambuliaji, huku wakihitaji kufanya marekebisho kwenye ulinzi ili kukabiliana na mashambulizi ya Yanga.
Matarajio ya Mechi ya Yanga Vs KMC Leo
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu kwa KMC kutokana na historia ya matokeo ya awali na hali ya sasa ya vikosi hivyo. Yanga inatarajiwa kuendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya KMC, huku mashabiki wa soka wakiwa na shauku kuona kama watetezi hao wa ubingwa wataendelea na mwenendo wao wa ushindi msimu huu. Kwa upande wa KMC, wana kibarua kigumu cha kuzuia mashambulizi ya Yanga na kutafuta namna ya kushambulia na kutikisa nyavu za Yanga, ambazo zimekuwa ngumu kupenyeza.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Septemba 29, 2024
- Dodoma Jiji Vs Simba Sc Leo 29/09/2024 Saa Ngapi
- Gomez Aanza Mikwara Ligi Kuu Bara, Aahidi Mabao Zaidi
- Kocha wa Kagera Sugar Matatani Baada ya Kipigo Kingine
- Viwango vya Mzize na Dube Vyampa Kazi Baleke Yanga
- FIFA Yaitandika Yanga Faini Nzito Kufuatia Kesi ya Okrah
Weka Komenti