Matokeo ya Darasa la Nne 2025 (NECTA Standard Four Results)

Matokeo ya Darasa la Nne 2025 (NECTA Standard Four Results)

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 10, 2026 limetangaza rasmi Matokeo ya Darasa la Nne 2025, kufuatia kukamilika kwa Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne uliofanyika tarehe 22 na 23 Oktoba 2025 katika shule zote za msingi nchini. Tangazo hili limetolewa baada ya Baraza kukamilisha mchakato wa uchunguzi, uhakiki na uthibitishaji wa matokeo kwa mujibu wa taratibu za kitaifa za mitihani.

Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne ni kipimo muhimu cha kitaaluma kinacholenga kutathmini kiwango cha umahiri, uelewa na maendeleo ya wanafunzi baada ya miaka minne ya elimu ya msingi. Matokeo ya upimaji huu hutumika kama rejea muhimu kwa serikali, walimu, wazazi na wadau wa elimu katika kupanga na kuboresha sera, mitaala na mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji.

Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa Darasa la Nne 2025

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya NECTA, jumla ya wanafunzi 1,583,686 walisajiliwa kushiriki Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne mwaka 2025. Kati yao:

  • Wasichana: 818,673 sawa na asilimia 52
  • Wavulana: 765,013 sawa na asilimia 48

Mahudhurio yalifikia asilimia 94, yakihusisha wanafunzi takribani 1.37 milioni kutoka shule za msingi 20,580 kote nchini. Aidha, wanafunzi 93,039 sawa na asilimia 6 hawakuhudhuria upimaji licha ya kusajiliwa, hali iliyotokana zaidi na utoro na changamoto za kiafya.

Ufaulu wa Jumla wa Darasa la Nne 2025

Kwa kuzingatia matokeo rasmi yaliyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzania, ufaulu wa jumla wa Darasa la Nne 2025 umefikia asilimia 88.91, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.67 ikilinganishwa na mwaka 2024. Jumla ya wanafunzi 1,249,970 walipata madaraja ya ufaulu ya A, B, C na D.

Kwa mlinganisho wa miaka ya nyuma:

  • 2023: Asilimia 83.34
  • 2024: Asilimia 86.24
  • 2025: Asilimia 88.91

Mwelekeo huu unaonesha kuimarika kwa ubora wa elimu ya msingi na utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa.

Ufaulu kwa Mujibu wa Jinsia

Takwimu zinaonesha kuwa:

  • Wasichana waliofaulu: Asilimia 90.1 ya wasichana wote waliofanya upimaji
  • Wavulana waliofaulu: Asilimia 87.59 ya wavulana wote

Kwa ujumla, kati ya wanafunzi wote waliofaulu:

  • Wasichana: 53%
  • Wavulana: 47%

Hali hii inaendelea kudhihirisha mchango chanya wa ushiriki wa wasichana katika elimu ya msingi.

Ufaulu kwa Shule

Kati ya shule 20,580 zilizoshiriki upimaji:

  • Shule 20,364 sawa na asilimia 99.3 zilipata wastani wa daraja la A hadi D
  • Shule 144 zilipata wastani wa daraja E, ambalo ndilo daraja la chini zaidi

Idadi ya shule zenye wastani wa daraja E imeendelea kupungua ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hali inayoonesha maboresho katika usimamizi na ufundishaji wa elimu ya msingi.

NECTA imeeleza kuwa matokeo ya wanafunzi waliokiuka kanuni za mitihani yamefutwa kwa mujibu wa sheria za mitihani za mwaka 2016. Hatua hizi zinalenga kulinda uadilifu na usawa wa mitihani ya taifa.

Matokeo ya Darasa la Nne 2025 NECTA SFNA Tanzania

Je, Matokeo ya Darasa la Nne 2025 Yatatangazwa Lini haswa?

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi Matokeo ya Darasa la Nne 2025 leo, tarehe 10 Januari 2026. Tangazo hilo limetolewa baada ya Baraza kukamilisha kikamilifu taratibu zote za kisheria na kitaalamu zinazohusisha ukaguzi, uhakiki na uthibitishaji wa matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne uliofanyika mwezi Oktoba 2025.

Kutangazwa kwa matokeo haya kunathibitisha kukamilika kwa majukumu ya Baraza kwa wakati, ikijumuisha uchambuzi wa kina wa takwimu za ufaulu, uhakiki wa matokeo kwa ngazi ya kitaifa, pamoja na maandalizi ya taarifa rasmi kwa ajili ya wadau wa elimu na umma kwa ujumla.

Wazazi, walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu wanapaswa kupata taarifa za matokeo haya kupitia tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) – www.necta.go.tz. Baraza linatoa tahadhari kwa umma dhidi ya matumizi ya vyanzo visivyo rasmi au taarifa zinazotolewa kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa yasiyoidhinishwa, ambazo zinaweza kupotosha na kukosa uhalali wa kitaasisi.

Rekodi za Kutangazwa Matokeo ya Darasa la Nne Miaka ya Nyuma

Kwa kutazama historia, matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili yamekuwa yakitangazwa kwa nyakati tofauti kulingana idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani na mchakato wa usahihishaji. Kwa mfano:

  • Mwaka 2024, matokeo ya mitihani wa darasa la nne yalitangazwa tarehe 4 Januari 2025.
  • Mwaka 2023, NECTA ilitangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili na Darasa la Nne (SFNA) tarehe 7 Desemba 2023.
  • Mwaka 2022, matokeo ya mitihani hii yalitangazwa tarehe 4 Januari 2023.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne 2025 NECTA Baada ya Kutangazwa

Baada ya matokeo ya mtihani wa Darasa la Nne 2025 kutangazwa rasmi na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), wanafunzi, wazazi, na walimu wanaweza kutazama kwa urahisi kwa kufuata hatua zifuatazo:

Hatua za Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne 2025 Kupitia Tovuti Rasmi ya NECTA

NECTA huchapisha matokeo kwenye tovuti yao rasmi. Hapa ndipo walimu, walezi na wanafunzi huyapata kwa haraka:

  1. Fungua kivinjari cha mtandao kwenye simu yako au kompyuta.
  2. Tembelea tovuti rasmi ya NECTA kwa kutumia anwani: www.necta.go.tz.
  3. Baada ya ukurasa wa mwanzo kufunguka, bonyeza sehemu ya “RESULTS” inayopatikana kwenye menyu kuu.
  4. Chagua “Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) 2025”.
  5. Ukurasa mpya utafunguka ukionyesha orodha ya mikoa yote ya Tanzania.
  6. Tutafuta Shule au Kituo chako
  7. Bonyeza jina la mkoa wako ili kufungua orodha ya wilaya zote ndani ya mkoa huo.
  8. Chagua wilaya ambayo shule yako inapatikana kwa kubonyeza jina la wilaya hiyo.
  9. Orodha ya shule na vituo vya mitihani vya wilaya hiyo itajitokeza.
  10. Tafuta jina la shule au namba ya kituo unachotaka, kisha bonyeza ili kuona matokeo ya wanafunzi wa shule hiyo.

Pia, Habariforum tumekurahisishia zaidi zoezi la kuangalia matokeo ya Darasa la Nne 2025 kwa kutoa viungo vya moja kwa moja (Direct Links). Viungo hivi vitakupeleka moja kwa moja kwenye kurasa za matokeo, hivyo kuepuka usumbufu wowote. Mara tu baada ya NECTA kutangaza matokeo, bonyeza jina la mkoa kwenye jedwali hapa chini ili kuona matokeo ya shule zote zilizopo katika mkoa husika.

ANGALIA HAPA CHINI MATOKEO YA DARASA LA NNE 2025

ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

Matokeo ya Darasa la Nne 2025 NECTA

Kuelewa Matokeo ya Darasa la Nne 2025

Baraza la mitihani Tanzania NECTA huyapanga matokeo ya mtihani wa darasa la nne kwa namna inayorahisisha ufahamu wa ufaulu wa wanafunzi katika masomo mbalimbali. Hapa Tumekuletea maelezo ya jinsi matokeo ya shule yatakavyoonekana baada ya kutangazwa

Muundo wa Matokeo ya darasa la nne

Matokeo ya Darasa la Nne yanajumuisha vipengele vifuatavyo:

Idadi ya Wanafunzi Walioshiriki Mtihani

Matokeo huonyesha jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani, idadi ya walioshiriki, na taarifa za wale ambao hawakuhudhuria.

Wastani wa Shule

Wastani wa alama ya shule yote hutolewa, ukionyesha kiwango cha jumla cha ufaulu wa wanafunzi wa shule husika. Hii pia inajumuisha daraja la wastani la shule, ambalo linaweza kuwa A, B, C, au D, kulingana na viwango vya ufaulu.

Madaraja ya Ufaulu: Matokeo yanatenganisha wanafunzi kulingana na madaraja yao ya ufaulu kwa ujumla:

  • A: Sifa ya Juu
  • B: Nzuri Sana
  • C: Nzuri
  • D: Inaridhisha
  • Referred: Wanafunzi waliokosa vigezo vya ufaulu

Matokeo ya Mwanafunzi Binafsi

Matokeo ya kila mwanafunzi huoneshwa kulingana na alama alizopata katika kila somo alilopimwa. Hapa huoneshwa:

  • Majina ya mwanafunzi na namba ya mtahiniwa.
  • Alama za kila somo.
  • Daraja lililopatikana kwa kila somo (kwa mfano, A, B, C, au D).
  • Wastani wa alama za jumla na daraja la jumla kwa mwanafunzi.

Ufaulu wa Masomo kwa Shule

Matokeo huonyesha muhtasari wa ufaulu wa masomo kwa shule nzima. Hii inajumuisha:

  • Idadi ya wanafunzi waliopata daraja tofauti (kwa mfano, waliopata A-D).
  • Wastani wa alama kwa kila somo, unaokadiriwa kwa kutumia alama za wanafunzi wote walioshiriki.
  • Daraja la wastani kwa kila somo (kwa mfano, Nzuri Sana, Nzuri, Inaridhisha).

Umuhimu wa Matokeo ya Darasa la Nne

Matokeo ya SFNA hutumika kutathmini si tu maendeleo ya wanafunzi, bali pia ubora wa elimu inayotolewa katika shule mbalimbali. Matokeo haya yanasaidia:

  • Wanafunzi: Kujua viwango vyao vya uelewa na maeneo yanayohitaji maboresho.
  • Walimu: Kuboresha mbinu za ufundishaji kulingana na changamoto zilizobainishwa.
  • Wazazi: Kuelewa maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao.
  • Wadau wa Elimu: Kuweka mikakati ya kuinua ubora wa elimu nchini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026
  2. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo vya VETA 2026
  3. When will 2025 Matric Results Released Online?
  4. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  5. Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
  6. Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026
  7. Form One Selection 2026 | Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo