Matokeo ya Fountain Gate Vs Kengold Fc Leo 11/09/2024 | Matokeo ya Fountain Gate Leo Dhidi ya Kengold Fc
Leo, tarehe 11 Septemba 2024, ligi kuu Tanzania bara (NBC premier league) inaendelea baada ya kupisha michezo ya ya kimataifa ambayo imekua ikifanyika kwa kipindi cha wiki mbili.
Mechi hii ya Fountain Gate Vs Kengold Fc inachezwa katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, mjini Babati, Manyara. Mchezo huu ni wa kihistoria kwa mkoa wa Manyara kwani ni mara ya kwanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania kufanyika katika ardhi ya mkoa huu.
Uwanja wa Tanzanite Kwaraa umeandaa mechi hii ya Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu mkoa wa Manyara ulipotengwa kutoka Arusha mwaka 2002. Fountain Gate FC iliamua kuutumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani kwa msimu huu wa 2024/2025, pamoja na Dodoma Jiji FC. Kwa wananchi wa Manyara, hususan Babati, huu ni mwanzo mpya wa soka katika mkoa ambao awali ulikuwa nyuma kisoka licha ya kuwa na utajiri wa rasilimali kama madini ya Tanzanite na vivutio vya kitalii kama Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ziwa Babati.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Babati (BDFA), Gerald Mtui, alisisitiza kuwa mechi hii si tu burudani, bali pia ni fursa ya kiuchumi kwa wafanyabiashara wa eneo hilo. Pia alielezea matumaini yake kuwa hamasa inayotokana na mechi hizi itasaidia kuimarisha timu za mkoa huu, hususan zile zinazoshiriki ligi za madaraja ya chini.
Kocha wa Fountain Gate FC, Mohamed Muya, alitoa shukrani kwa sapoti kubwa waliyoipata kutoka kwa wakazi wa Babati na mkoa wa Manyara kwa ujumla. Hii imetoa nguvu zaidi kwa timu yake kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Kengold FC.
Matokeo ya Fountain Gate Vs Kengold Fc Leo 11/09/2024
Fountain Gate | 2-1 | Kengold Fc |
Mapendekezo ya Mhariri;
Weka Komenti