Matokeo ya JKT Tanzania vs Simba Leo 08/11/2025
Simba SC leo inashuka dimbani ikisaka pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania, katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni. Mchezo huu unaonekana kuwa wa kimkakati kwa pande zote mbili, huku kila timu ikihitaji ushindi ili kujiimarisha katika mbio za ubingwa wa msimu huu.
Ligi Kuu Bara inarejea kwa hamasa kubwa baada ya mapumziko mafupi, huku presha ya ushindani ikiendelea kupanda kileleni. Kabla ya mchezo huu, vinara wa msimamo ni Mbeya City wenye pointi nane, na hivyo kuifanya mechi hii kuwa na uzito wa moja kwa moja katika mabadiliko ya msimamo wa juu wa ligi.
Simba: Lengo ni Ushindi na Mabao
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinaingia uwanjani kikiwa na alama sita baada ya kushinda michezo miwili mfululizo kwa mabao 3–0 dhidi ya Fountain Gate na Namungo. Kocha wa Simba, Selemani Matola, amesema bayana kuwa mkakati wa timu yake si ushindi pekee, bali ushindi wa mabao ya kuridhisha.
“Tumejipanga kuhakikisha tunakwenda katika mchezo huu kupata pointi tatu na kufunga bao zaidi ya moja. Tunafahamu mpinzani ana timu ngumu kutokana na uwepo wa wachezaji wenye uzoefu,” Selemani Matola, Kocha Mkuu Simba.
Beki wa timu hiyo, Wilson Nangu, alisisitiza dhamira hiyo ya ushindi akisema:
“Tumefanya maandalizi ya kutosha ili kwenda kushinda mechi ya kesho. Tunafahamu ugumu ambao tutakutana nao, ila naamini tutakuwa bora zaidi na kutimiza lengo la kupata pointi tatu.”
Simba inatarajiwa kuwategemea nyota wake muhimu kama Jonathan Sowah, Selemani Mwalimu, Jean Charles Ahou na Steven Mukwala, huku safu ya ulinzi ikiongozwa na Rushine de Reuck, Chamou Karaboue na Wilson Nangu.
Hata hivyo, kikosi hicho kitapungukiwa na baadhi ya wachezaji muhimu wakiwemo kipa namba moja Moussa Camara na beki Abdulrazak Hamza kwa majeraha, wakati hali ya kiungo Mohammed Bajaber bado ina utata wa kucheza.
Kwa upande wa JKT Tanzania, timu hiyo inashuka dimbani ikiwa na pointi saba baada ya michezo mitano dhidi ya Mashujaa FC, Coastal Union, Mbeya City, Namungo FC na Azam FC. Licha ya kutokuwa na mwanzo mbaya msimu huu, rekodi haijawa upande wao kila wanapokutana na Simba.
Katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Simba, JKT imefungwa zote, ikiruhusu jumla ya mabao sita bila ya kujibu. Pia, katika michezo miwili iliyochezwa kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Simba iliibuka na ushindi katika yote.
Hata hivyo, Wanajeshi wanayo silaha kali katika safu ya ushambuliaji, wakitegemea vinara wa mabao wa ligi hadi sasa Paul Peter na Saleh Karabaka, wakisaidiwa na Hassan Dilunga pamoja na Edward Songo.
Matokeo ya JKT Tanzania vs Simba Leo 08/11/2025
| JKT Tanzania | VS | Simba |
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Ligi Kuu Wanawake Tanzania (TWPL) 2025/2026
- Droo ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
- Yanga Yaangukia Kundi B na Al Ahly Droo ya Makundi Klabu Bingwa 2025/2026
- Msimamo Kundi la Yanga Klabu Bingwa 2025/2026
- Msimamo Kundi la Simba Klabu Bingwa 2025/2026
- Droo ya Makundi Klabu Bingwa Afrika 2025/2026









Leave a Reply