Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results)

Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results)

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linatarajiwa kutangaza Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026, yanayojulikana rasmi kama Form Two National Assessment (FTNA), kwa wanafunzi wote waliofanya mtihani wa upimaji wa kitaifa wa Kidato cha Pili katika shule za sekondari nchini Tanzania. Matokeo haya ni sehemu muhimu ya tathmini ya kitaaluma, yakilenga kupima kiwango cha uelewa wa wanafunzi baada ya miaka miwili ya masomo ya sekondari na kutoa mrejesho muhimu kwa wanafunzi, walimu, wazazi na wadau wengine wa elimu.

Mtihani wa FTNA ni tathmini endelevu inayolenga kufuatilia maendeleo ya ujifunzaji wa mwanafunzi, badala ya kuwa mtihani wa ushindani. Kupitia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026, mfumo wa elimu hupata fursa ya kubaini mafanikio, changamoto na maeneo yanayohitaji maboresho kabla ya mwanafunzi kuendelea na Kidato cha Tatu.

Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results)

Mtihani wa Upimaji wa Kidato Cha Pili (FTNA) ni Nini?

Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili, maarufu kama FTNA, ni mtihani wa kitaifa unaosimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa wanafunzi wa shule zote za sekondari nchini. Mtihani huu hufanyika kila mwaka na hutumika kama chombo muhimu cha tathmini ya kielimu kinachopima kiwango cha maarifa na uelewa wa mwanafunzi katika masomo ya msingi ya sekondari.

Kwa mwaka 2025, mtihani wa upimaji wa Kidato cha Pili ulifanyika katika shule zote za sekondari nchini Tanzania kuanzia tarehe 10 Novemba 2025 hadi 20 Novemba 2025. Kipindi hiki kilihusisha tathmini ya kina ya masomo mbalimbali yaliyomo kwenye mtaala wa elimu ya sekondari, kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya ujifunzaji wa wanafunzi baada ya miaka miwili ya masomo.

Mtihani wa Upimaji wa kidato cha pili (FTNA) ni tathmini endelevu inayolenga kutoa mrejesho unaoweza kutumika na walimu kuboresha mbinu za ufundishaji, wanafunzi kuongeza juhudi katika maeneo yenye changamoto, pamoja na wazazi na walezi kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao kabla ya kuendelea na Kidato cha Tatu.

Soma Pia

  1. Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026
  2. Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
  3. Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)
  4. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026
  5. Siku ya Kuripoti Shule Kidato cha Kwanza 2026

Masomo Yaliousika Katika Mtihani wa Kidato Cha Pili 2025

Mtihani wa Kidato Cha Pili unahusisha masomo mbalimbali yanayolenga kukuza maarifa ya kinadharia pamoja na ujuzi wa vitendo. Masomo hayo ni pamoja na:

  • Kiswahili
  • Basic Mathematics
  • English Language
  • Biolojia
  • Fizikia
  • Kemia
  • Jiografia
  • Historia
  • Uraia
  • Elimu ya Dini ya Kiislamu
  • Bible Knowledge
  • Masomo ya Ufundi kama Building Construction, Mechanical Engineering na Electrical Engineering
  • Masomo ya Biashara kama Book-Keeping na Commerce
  • Lugha za Kigeni kama Kifaransa na Kichina

Mchanganyiko huu wa masomo unaakisi malengo ya elimu ya sekondari nchini Tanzania katika kujenga wanafunzi wenye maarifa mapana na ujuzi unaoendana na mtaala wa taifa.

Je, NECTA Imeshatangaza Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026?

Hadi sasa, NECTA bado haijatangaza rasmi Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 wala kutoa taarifa kuhusu tarehe kamili ya kutolewa kwa matokeo hayo. Hakujakuwa na tamko rasmi linaloeleza siku au muda mahsusi wa kutangazwa kwa matokeo ya FTNA.

Hata hivyo, kwa kuzingatia utaratibu wa miaka ya nyuma, Matokeo ya Kidato Cha Pili kwa kawaida hutangazwa mwanzoni mwa mwezi Januari, baada ya kukamilika kwa taratibu zote za uchakataji na uhakiki wa matokeo.

Wanafunzi, wazazi na walezi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa kupitia tovuti rasmi ya NECTA ambayo ni https://necta.go.tz

NECTA FTNA Results 2025/2026: Nini Kinaonyeshwa Kwenye Matokeo?

Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results) huonesha kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi kwa kila somo pamoja na daraja la jumla (Division). Aidha, matokeo haya huwasilishwa kwa kuzingatia mgawanyo wa kijinsia, jambo linalosaidia kutoa picha ya hali ya elimu kitaifa kwa mwaka husika.

Muonekano wa Ukurasa wa Matokeo ya Kidato Cha Pili

Kwa wanafunzi na wazazi, taarifa hizi ni muhimu katika kufanya maamuzi ya kitaaluma, hususan wakati wa kuchagua mwelekeo wa masomo pindi mwanafunzi anapoendelea na Kidato cha Tatu.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 Mtandaoni

Baada ya Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results) kutangazwa rasmi na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), wanafunzi, wazazi na walezi wanaweza kuyapata kwa urahisi kupitia mtandao. NECTA hutoa matokeo haya kupitia tovuti yake rasmi, hatua inayolenga kuhakikisha uwazi na upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati.

Ili kusaidia kuelewa kwa vitendo mchakato wa kuangalia matokeo, video ifuatayo inaonesha hatua za kufuata wakati wa kuangalia NECTA FTNA Results 2025/2026 mtandaoni.

Hatua za Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026

Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA
Fungua kivinjari cha intaneti na nenda kwenye tovuti rasmi ya NECTA. Hakikisha una muunganisho mzuri wa intaneti ili kurahisisha upakiaji wa ukurasa wa matokeo.

Bofya Sehemu ya “Results”
Baada ya kufungua tovuti, bofya menyu ya Results ambapo mitihani yote ya kitaifa huorodheshwa.

Chagua FTNA (Form Two National Assessment)
Tafuta na ubofye kipengele cha FTNA ili kufungua ukurasa wa Matokeo ya Kidato Cha Pili.

Chagua Mwaka wa Mtihani 2025
Chagua mwaka husika ili kupata Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025/2026 (NECTA FTNA Results).

Tafuta Jina la Shule
Orodha ya shule zote zilizoshiriki mtihani itaonekana. Tafuta jina la shule unayotaka kuangalia matokeo yake.

Tafuta Namba ya Mtihani ya mwanafunzi
Ndani ya ukurasa wa shule, unaweza kutafuta jina la mwanafunzi au namba ya mtihani ili kuona matokeo yake binafsi, ikiwemo alama za masomo, jumla ya alama na daraja la ufaulu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Darasa la Nne 2025/2026 (NECTA SFNA Results)
  2. NECTA Yatangaza Usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE na FTNA 2026
  3. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  4. Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo