Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 (NECTA Form Six Results 2024)
Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 YATANGAZWA RASMI
Breaking news. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha sita leo july 13 2024, huku matokeo ya watahiniwa 24 kati ya watahiniwa 113, 536 yakifutwa kutokana na udanganyifu. Dk Said Mohamed amesema watahiniwa walibainika kuingia na simu kwenye vyumba vya mtihani, kukutwa na notisi na wengine kusaidiana kufanya mitihani.
Ufaulu; Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 (NECTA Form Six Results 2024)
Dk Mohamed amesema kuwa jumla ya watahiniwa 113,536 kutoka shule na kujitegemea walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Mei mwaka huu. Kati ya hao, wasichana walikuwa 50,614 (44.58%) na wavulana 62,922 (55.42%).
Idadi ya Watahiniwa na Matokeo Yao
Kati ya watahiniwa hao, 104,454 walikuwa wa shule na 9,082 walikuwa wa kujitegemea. Dk Mohamed alibainisha kuwa kati ya watahiniwa 104,454 wa shule, 103,812 (99.39%) walifanya mtihani. Wasichana walikuwa 46,793 (99.43%) na wavulana 57,019 (99.35%). Watahiniwa 642 (0.61%) hawakufanya mtihani.
Ufaulu wa Jumla wa Mtihani
Kwa mujibu wa Dk Mohamed, watahiniwa wa shule waliofaulu ni 103,252 (99.92%). Kati ya hao, wasichana waliofaulu ni 46,615 (99.93%) na wavulana 56,637 (99.91%). Watahiniwa 84 (0.08%) walishindwa mtihani. Ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 96,319 (99.44%), mwaka 2024 kumekuwa na ongezeko la asilimia 7.78 ya watahiniwa waliofanya mtihani.
Uongozi wa Wasichana katika Ufaulu
Watahiniwa 111,056 (99.43%) walifaulu mtihani wa kidato cha sita 2024. Kati ya hao, wasichana waliofaulu ni 49,837 (99.61%) na wavulana 61,219 (99.28%). Mwaka 2023 watahiniwa waliofaulu walikuwa 104,549 (99.23%), hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.20 ikilinganishwa na mwaka 2023.
Ubora wa Ufaulu kwa Madaraja
Ubora wa ufaulu kwa kuzingatia madaraja unaonesha kuwa watahiniwa 102,719 (99.40%) walipata madaraja I-III. Watahiniwa wengi walipata Daraja la I na II, ambapo Daraja la I walikuwa 47,862 (46.32%) na Daraja la II walikuwa 42,359 (40.99%). Mwaka 2023, watahiniwa waliopata madaraja I-III walikuwa 95,442 (99.30%), hivyo ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.10.
Ufaulu wa Tahasusi za Lugha, Sayansi Jamii, Biashara na Uchumi
Asilimia 94.20 hadi 95.95 ya watahiniwa walipata ufaulu wa Daraja la I-II katika tahasusi za Lugha, Sayansi Jamii, Biashara na Uchumi, huku asilimia 79.40 wakifaulu katika tahasusi za Sayansi Asilia. Asilimia 66.69 ya watahiniwa walipata Daraja la III katika tahasusi za ualimu wa masomo ya sayansi na biashara. Idadi kubwa ya watahiniwa waliopata Daraja la I-II ipo katika tahasusi za Sayansi Asilia (31,386) ikifuatiwa na tahasusi za Sayansi Jamii (30,126).
Kuhusu Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 (NECTA Form Six Results 2024)
Matokeo ya kidato cha sita ni matokeo ya mtihani wa kidato cha sita ambao hufanyika mashuleni kote baada ya kuhitimisha miaka miwili ya elimu ya sekondari ya A-Level. Mitihani hii hufanyika kila mwaka na msimu wa elimu wa 2023, mitihani ya kidato cha sita 2023 ya NECTA ilianza kufanyika tarehe 6 Mai 2024 na kumalizika tarehe 24 Mei 2024. Matokeo haya yana athari kubwa katika maisha ya wanafunzi kwani yanaamua hatma yao ya kujiunga na vyuo vikuu, vyuo vya ufundi, au kujiingiza moja kwa moja katika soko la ajira.
Kwa wanafunzi wengi, matokeo kidato cha sita 2024 yatakua ni hatua muhimu katika kufikia malengo yao ya kielimu na kitaaluma. Wazazi na walimu nao pia wanayafuatilia kwa karibu kwani wana jukumu kubwa katika kuhakikisha wanafunzi wanapata matokeo bora. Aidha, matokeo haya yanatoa taswira ya ubora wa elimu katika shule mbalimbali na mikoa tofauti nchini Tanzania.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2024
1. Tembelea Tovuti ya NECTA
Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.necta.go.tz.
2. Nenda kwenye Menyu ya Tovuti na Bonyeza “Matokeo”
Katika ukurasa wa kwanza wa tovuti ya NECTA, nenda kwenye menyu kuu na bonyeza kipengele cha “Matokeo.”
3. Chagua “Matokeo ya ACSEE”
Kutoka kwenye orodha ya matokeo, chagua “Matokeo ya ACSEE” ambayo ni matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita.
4. Bonyeza “Matokeo ya ACSEE 2024”
Ukurasa wa Matokeo ya ACSEE utafunguka, bonyeza “Matokeo ya ACSEE 2024” kuona matokeo ya mwaka 2024.
5. Tafuta Shule Yako
Ukurasa wa “Utafutaji wa Matokeo ya Mtihani wa ACSEE 2024” utafunguka. Tafuta jina la shule yako kutoka kwenye orodha iliyopo.
6. Bonyeza Kiungo cha Shule Yako
Bonyeza kiungo cha shule yako ili kuona matokeo yake. Ili kupata matokeo yako binafsi, fungua kiungo cha shule yako kisha tafuta jina lako baada ya ukurasa wa matokeo ya shule kufunguka.
Hatua za Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 Kupitia USSD
- Piga *152*00#
- Chagua namba 8. ELIMU
- Chagua namba 2. NECTA
- Chagua aina ya huduma 1. MATOKEO
Chagua aina ya Mtihani 2. ACSEE - Ingiza Namba ya Mtihani na Mwaka Mfano: S0334-0556-2019
- Chagua aina ya Malipo (Gharama kwa SMS ni Tshs 100/=)
- Baada ya kukamilisha malipo, utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo.
ANGALIA HAPA Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 (NECTA Form Six Results)
ALL CENTRES | A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M |
N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z |
All School Form Six Results 2024
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti