Matokeo ya Simba vs Dodoma Jiji Leo 25/02/2026

Matokeo ya Simba vs Dodoma Jiji Leo 25/02/2026

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo wanatarajiwa kushuka katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kuwakabili wenyeji Dodoma Jiji FC katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC. Mchezo huu wa Februari 25, 2026, unaangaliwa kwa jicho la kipekee kutokana na historia ya matokeo baina ya timu hizi pamoja na presha ya msimamo wa ligi. Mashabiki wanasubiri kwa hamu Matokeo ya Simba vs Dodoma Jiji Leo 25/02/2026, mechi inayochezwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Jamhuri uliopo jijini Dodoma. Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya nne na pointi 22, huku ikiwa imeachwa kwa pointi tatu na watani zao wa jadi. Kwa upande mwingine, Dodoma Jiji ina pointi 20 baada ya kucheza mechi 15. Ushindi kwa Dodoma Jiji leo unaweza kuipandisha hadi nafasi ya nne, ikiishusha Simba kutoka nafasi hiyo. Hii inaifanya mechi ya leo kuwa na uzito mkubwa katika mbio za juu ya msimamo wa ligi. Matokeo ya Simba vs Dodoma Jiji Leo 25/02/2026

Fuatilia Hapa Matokeo ya Simba vs Dodoma Jiji Leo 25/02/2026

Uimara wa Nyumbani dhidi ya Rekodi ya Ugenini

Chini ya Kocha Aman Josiah, Dodoma Jiji imeonyesha uthabiti mkubwa katika Uwanja wa Jamhuri. Katika mechi saba za nyumbani msimu huu, imepoteza moja pekee ilipofungwa 3-0 na Pamba Jiji, huku ikishinda nne na kutoka sare mbili. Takwimu hizi zinaipa ujasiri wa kujaribu kuvunja uteja dhidi ya Simba. Kwa upande wa Simba, rekodi ya ugenini msimu huu ni thabiti. Imecheza mechi tatu za ligi ugenini na kushinda zote dhidi ya JKT Tanzania (2-1), KMC (2-0) na Tanzania Prisons (2-0). Aidha, tangu ipoteze 1-0 ugenini dhidi ya Esperance Januari 25, 2026 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imeshuka dimbani mara saba mfululizo bila kupoteza katika mashindano yote. Katika kipindi hicho imepata ushindi dhidi ya Mashujaa, KMC, Tanzania Prisons, Stade Malien na Greenland, huku ikitoa sare dhidi ya Esperance na Petro Atletico. Mfululizo huo unaashiria uthabiti wa kikosi hicho kuelekea mchezo wa leo.

Historia Ya Mikutano

Tangu msimu wa 2020/2021, Simba imekuwa na rekodi ya ushindi wa asilimia mia moja dhidi ya Dodoma Jiji kwenye ligi, ikishinda mechi zote kumi walizokutana. Msimu uliopita, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 6-0 jijini Dar na baadaye kushinda 1-0 Dodoma, na kufanya jumla ya mabao kuwa 7-0 katika msimu huo. Takwimu hizi zinaweka presha kwa Dodoma Jiji, hasa ikizingatiwa kuwa inacheza nyumbani.

Taarifa za Kikosi

Mchezo wa leo ni wa mwisho kwa wachezaji wa Simba, Jonathan Sowah na Allasane Kante, kukosekana kutokana na adhabu ya mechi tano mfululizo za Ligi Kuu Bara. Wawili hao waliadhibiwa Desemba 17, 2025 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kufuatia makosa ya kinidhamu katika mechi dhidi ya Azam FC ya Desemba 7, 2025. Wanatarajiwa kurejea katika mchezo dhidi ya Yanga Machi 1 mwaka huu.

Kauli ya Kocha

Kocha wa Simba, Steve Barker, alieleza kuwa kikosi chake kimejiandaa kwa changamoto ya leo.

“Tumejipanga vizuri, mpinzani wetu wa leo ni mzuri. Tumeanza kuonyesha matokeo mazuri ya mfululizo na tunaendelea kujiimarisha katika utengenezaji wa nafasi na kuzitumia kupata ushindi. Mechi ya leo itakuwa ngumu, lakini tumejiandaa kukabiliana na hali yoyote.”

Aliongeza kuwa hatarajii mchezo mwepesi, akisisitiza kuwa timu bora ndiyo itakayoibuka na ushindi. Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB FA CUP 2025/26
  2. Kocha Steve Barker Aeleza Mkakati wa Simba Katika Mechi Tatu Zijazo
  3. Kocha Yusuf Chipo Alia na Mabeki Baada ya Mtibwa Kufungwa 3-1 na Singida BS
  4. Droo ya Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Kufanyika Februari 24
  5. Mgombea Urais Barcelona Victor Font Aahidi Kumrejesha Messi Camp Nou

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo