Matokeo ya Simba VS Es Tunis Leo 1/02/2026
Leo saa 10:00 jioni, klabu ya Simba SC itashuka dimbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuikaribisha Esperance de Tunis katika mechi ya marudiano ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huu utarushwa mbashara kupitia Azam Sports 1 HD, huku macho ya mashabiki yakielekezwa kwenye hatima ya Simba katika Kundi D.
Kwa Simba, mechi ya leo ni ya uamuzi wa moja kwa moja. Matokeo yoyote tofauti na ushindi yatamaanisha safari yao katika mashindano haya kufikia tamati. Simba inaingia ikiwa haina pointi, ikiburuta mkia wa kundi, hali inayolazimisha ushindi wa lazima ili kuendelea kushikilia matumaini ya kufuzu robo fainali. Ikiwa Simba itashinda, itabaki na nafasi ya kusonga mbele, lakini italazimika pia kushinda mechi mbili zilizobaki na kuomba matokeo ya wapinzani wengine yawe na manufaa kwao.
Kumbukumbu ya Mchezo wa Kwanza
Mchezo wa kwanza kati ya timu hizi ulipigwa Januari 24, 2026, ambapo Esperance iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Ushindi wa leo kwa Simba hautakuwa tu wa pointi tatu, bali pia kisasi cha kipigo cha awali.
Kauli za Benchi la Ufundi
Kocha wa Simba, Steve Barker, alisisitiza uzito wa mchezo huu:
“Tunajua kwamba tunacheza dhidi ya timu nzuri. Tunaamini bado nafasi ipo kwa sababu tutakuwa nyumbani na tukiungwa mkono na mashabiki wetu. Ili tupate ushindi, tunatakiwa kutumia vizuri nafasi tunazotengeneza.”
Aliongeza kuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika hakuna timu rahisi, hivyo nidhamu na umakini ni vitu vya msingi.
Morali ya Wachezaji
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Morice Abraham, alisema wachezaji wote wako tayari kwa kazi kubwa:
“Ni mchezo ambao tunahitaji matokeo ya ushindi pekee. Morali iko juu kwa sababu kila mmoja anajua umuhimu wa mchezo huu. Tumeanza vibaya lakini tuna nafasi ya kumaliza vizuri.”
Kauli hii inaakisi dhamira ya kikosi kizima cha Simba, ambacho kinahitaji kushinda mechi tatu zilizobaki ili kufikisha pointi tisa zinazoweza kuwavusha robo fainali.
Msimamo wa Kundi D
Katika Kundi D:
- Simba: haina pointi.
- Esperance: ina pointi tano.
- Stade Malien: pointi saba.
- Petro Atletico: pointi nne.
Kwa Esperance, hata sare leo ina faida, kwani itafikisha pointi sita na kujiweka karibu zaidi na hatua ya robo fainali.
Fuatlia Hapa Matokeo ya Simba VS Es Tunis Leo 1/02/2026
| Simba SC | 2-2 | ES Tunis |
Mabadiliko ya Kikosi cha Simba
Simba imeingia kwenye mechi hii ikiwa na nguvu mpya baada ya kusajili nyota sita wa kigeni:
- Jospin Loemba
- Libasse Gueye
- Anicet Oura
- Clatous Chama
- Djibrilla Kassali
- Ismael Toure
Usajili huu umeanza kuonyesha matunda, hasa baada ya Simba kuifunga Mashujaa 2-0 katika Ligi Kuu Bara, ambapo Libasse Gueye alifunga bao la kwanza na Seleman Mwalimu kuongeza la pili.
Rekodi na Historia
Tangu mwaka 2018, Simba haijawahi kuishia hatua ya makundi katika mashindano ya CAF. Kila mara imekuwa ikivuka kwenda robo fainali, na msimu wa 2024–2025 ilifika hadi fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hata hivyo, rekodi zinaonyesha kuwa hakuna timu iliyowahi kupoteza mechi tatu za mwanzo za makundi kisha ikafuzu robo fainali, jambo linaloongeza presha kwa Simba.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply