Matokeo ya Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025
Klabu ya Simba SC leo itatinga dimbani kwa mara ya pili katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kuvaana na Namungo, mchezo utakaopigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam saa 2:15 usiku. Huu utakuwa mchezo muhimu kwa Wekundu wa Msimbazi ambao wataingia uwanjani bila Kocha Mkuu baada ya kuondoka kwa Fadlu Davids, huku majukumu ya kuongoza benchi la ufundi yakibebwa na Seleman Matola. Upande wa pili, Namungo itaongozwa na kocha wake Juma Mgunda, ambaye ana historia ya kuifundisha Simba.
Simba SC imekuwa ikijipanga kwa umakini kuelekea mchezo huu, ikilenga kuendeleza rekodi yake nzuri dhidi ya Namungo. Timu hiyo imeanza msimu kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate, mchezo ambao pia uliendeshwa na Matola.
Akizungumza kabla ya pambano, Matola alikiri kuwa licha ya rekodi nzuri walizonazo, mechi dhidi ya Namungo si rahisi:
“Tunatarajia kuwa na mechi ngumu. Kama ukiangalia rekodi, Namungo wamekuwa wakitusumbua licha ya kwamba tumewafunga mechi mbili za mwisho. Wana kocha mzuri anayeifahamu Simba, hivyo tutaingia uwanjani na tahadhari kubwa,” alisema Matola.
Changamoto kubwa kwa Simba imekuwa kushindwa kutumia nafasi nyingi wanazozitengeneza. Hata hivyo, Matola alibainisha kuwa wamelifanyia kazi hilo ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya katika mchezo huu wa leo.
Kwa upande wa Namungo, Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano, licha ya kukutana na timu kubwa yenye wachezaji wa kiwango cha juu.
“Tumejiandaa vizuri kukutana na Simba. Tunaijua ni timu nzuri yenye wachezaji bora, lakini tumekuja kushindana nao na tupo tayari kupambana kupata matokeo,” alisema Mgunda.
Namungo imeanza msimu huu vizuri ikicheza michezo miwili, ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya Pamba Jiji na kushinda 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons. Hii imewapa morali kuelekea mchezo wa leo.
Matokeo ya Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025
Simba Sc | VS | Namungo |
Rekodi za Simba dhidi ya Namungo
Historia ya mechi kati ya Simba SC na Namungo FC inazipa nguvu zaidi Wekundu wa Msimbazi. Takwimu zinaonyesha kuwa katika michezo 13 ya mashindano iliyowakutanisha timu hizi, Simba imeshinda mara nane (8), huku mingine mitano (5) ikiisha kwa sare. Hakuna mchezo ambao Namungo amewahi kushinda.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana msimu uliopita, Simba ilishinda nyumbani na ugenini bila kuruhusu bao. Kabla ya hapo, timu hizo zilimaliza kwa sare tatu mfululizo, ishara kwamba Namungo huwa si mpinzani mwepesi. Hata hivyo, kumbukumbu zinaonyesha kuwa hata kwenye Kombe la FA Januari 2021, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025
- Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025 Saa Ngapi?
- Singida BS Yaendeleza Ubabe Mbele ya Mashujaa na Kubaki Kinara wa Ligi Kuu Bara
- Ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
- Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
- Yanga Sc Yalazimishwa Sare Ya 0-0 Na Mbeya City
- Ratiba ya Mechi za Leo 30/09/2025 Ligi Kuu ya NBC
- Ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
Leave a Reply