Man City Washinda Ngao ya Jamii 2024 Baada ya Kuichapa Man United Kwa Penalti
Katika kile kilichoonekana kama onyesho la kusisimua la soka la Uingereza, Manchester City iliibuka kidedea kwa kuinyuka Manchester United kwa mikwaju ya penalti 7-6 na kutwaa Ngao ya Jamii ya mwaka 2024, baada ya sare ya 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo uliosakatwa kwenye Uwanja wa Wembley Jumamosi iliyopita.
Kipindi cha kwanza cha mchezo kilikuwa na ushindani mkali kutoka pande zote mbili, huku kila timu ikionyesha nia ya kutaka kuandika bao la mapema, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda. Iliwabidi mashabiki kusubiri hadi dakika ya 82 ndipo mchezaji aliyeingia akitokea benchi, Alejandro Garnacho, mshindi wa Copa America 2024, alipopachika bao la kwanza kwa upande wa Man United na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Mashetani Wekundu.
Hata hivyo, furaha ya mashabiki wa Man united haikudumu kwa muda mrefu. Dakika chache kabla ya kipenga cha mwisho cha dakika 90, Bernardo Silva, ambaye anasherehekea siku ya kuzaliwa leo 10 Agosti, alifunga bao la kusawazisha kwa kichwa maridadi akimalizia krosi safi kutoka kwa Oscar Bobb na kuipeleka mechi kwenye mikwaju ya penalti.
Katika mikwaju ya penalti, kila timu ilipata nafasi ya kuonyesha umahiri wake. Wachezaji wote walionyesha umahiri wao wa kupiga penalti, lakini hatimaye ilikuwa ni Matheus Nunes wa Manchester City aliyefunga penalti ya ushindi, na kuizamisha Manchester United kwenye dimbwi la majonzi.
Ushindi huu ni kisasi kitamu kwa vijana wa Pep Guardiola, ambao walikuwa wamelazwa 2-1 na Man United kwenye fainali ya Kombe la FA 2024 miezi michache iliyopita.
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza unatarajiwa kuanza tarehe 18 Agosti, ambapo Manchester City itaanza safari yake ya kutetea ubingwa wake kwa kucheza dhidi ya Chelsea. Mashabiki wa soka kote ulimwenguni wanasubiri kwa hamu kuanza kwa msimu mpya, wakitarajia burudani zaidi na ushindani mkali kutoka kwa timu zote zinazoshiriki.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Hizi apa Picha za Jezi Mpya ya KMC Fc 2024/2025
- Viingilio Mechi ya Fainali ya Yanga Vs Azam Fc Ngao Ya Jamii 2024
- Waamuzi Watakao chezesha Yanga SC vs Azam Ngao ya Jamii 2024: Hawa Hapa!
- Ratiba ya Simba Sc Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
- Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
- Ratiba ya Fainali Ngao Ya Jamii 2024
- Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024
Weka Komenti