Matokeo ya Taifa Stars vs Morocco Leo 22/08/2025 CHAN
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo kitashuka dimbani kupambania nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya CHAN 2024 ambapo kitachuana na mabingwa wa soka barani Afrika, Morocco, katika mtanange wa kukata shoka unaotarajiwa kutimua vumbi katika dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam majira ya saa 2:00 usiku.
Mashabiki wa soka kote nchini wanasubiri kwa hamu matokeo ya Taifa Stars vs Morocco leo 22/08/2025 CHAN ili kuona kama Stars wataandika historia mpya ya kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza.
Maandalizi ya Taifa Stars Kabla ya Mchezo
Nahodha wa Taifa Stars, Dickoson Job, amethibitisha kuwa kikosi kipo tayari kwa changamoto hii kubwa na kimejipanga vyema kisaikolojia na kimwili. Akizungumza kabla ya mchezo, Job alisema:
“Tunajua tunakutana na timu ngumu yenye uzoefu mkubwa, lakini tumewachambua tangu mwanzo wa mashindano. Tupo tayari na tunaahidi kupambana kwa nguvu zote ili kuwaletea Watanzania matokeo chanya,” alisema Job.
Amesisitiza nidhamu ya mchezo, umakini na kutumia kila nafasi watakayopata ili kuandika historia mpya kwenye michuano ya CHAN.
Mbinu za Kocha Hemed Suleiman
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman, ameweka wazi kuwa Stars wataingia uwanjani wakiwa na mbinu za kiufundi za kujilinda kwa nidhamu huku wakishambulia kwa ufanisi kila watakapopata nafasi.
Suleiman alikumbusha jinsi Stars walivyofanya vizuri hatua ya makundi kwa kufunga mabao matano na kuruhusu bao moja pekee, rekodi ambayo imewapa heshima kubwa na kuwatia wachezaji morali wa hali ya juu.
“Tunatakiwa kutumia kila nafasi vizuri huku tukihakikisha hatupati makosa nyuma. Mashabiki wetu ni wachezaji wa 12, tunahitaji sapoti yao kubwa leo usiku,” alisema Suleiman.
Matokeo ya Taifa Stars vs Morocco Leo 22/08/2025 CHAN
Tanzania | VS | Morocco |
Friday, August 22, 2025
👕 | Tanzania 🇹🇿 ✖ 🇲🇦 Morocco
🏆 | CHAN 2024 – Quarter-finals
⏰ | 20:00 🇹🇿
🏟️ | Benjamin Mkapa Stadium – Dar Es Salaam
Safari ya Taifa Stars na Morocco Kufika Robo Fainali
Tanzania ilimaliza kileleni mwa Kundi A ikiwa na pointi 10 baada ya kushinda mechi tatu na kutoka sare moja, rekodi ambayo imewapa nafasi ya kipekee kwenye robo fainali.
Kwa upande wa Morocco, walimaliza nafasi ya pili Kundi A wakiwa na pointi 9, wakishinda mechi tatu na kupoteza moja dhidi ya Kenya. Waliwafunga Angola 2-0, wakaangukia kwa Kenya 0-1, kisha kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Historia ya Taifa Stars dhidi ya Morocco
Mchezo wa leo utakuwa ni mara ya nane kwa Taifa Stars na Morocco kukutana kwenye mashindano rasmi. Morocco wana rekodi nzuri zaidi wakiwa wameshinda michezo sita, huku Tanzania ikishinda mchezo mmoja pekee na hakuna sare kati ya timu hizo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Taifa Stars vs Morocco Leo 22/08/2025 CHAN
- Cv ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026
- Wafungaji Bora CHAN 2025
- Tanzania Vs Morocco Chan 22/08/2025 Saa Ngapi?
- Jonathan Sowah Kuikosa Simba vs Yanga Ngao ya Jamii Septemba 16, 2025
- Sherehe za Wiki ya Mwananchi 2025 Yanga Day Kufanyika Benjamin Mkapa Septemba 12
- Khalid Aucho Asaini Mkataba wa Miaka 2 na Singida Black Stars
- Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025 | Mechi za Robo fainali CHANI
Leave a Reply