Matokeo ya Tanzania Taifa Stars vs Morocco Leo 04/01/2026

Matokeo ya Tanzania Taifa Stars vs Morocco Leo 04/01/2026

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania, Taifa Stars, leo itashuka katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, jijini Rabat, kuivaa Morocco katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, ukiwa na uzito mkubwa kwa pande zote mbili huku ukifungua ukurasa mpya katika historia ya soka la Tanzania.

Matokeo ya Tanzania Taifa Stars vs Morocco Leo 04/01/2026

Huu ni mchezo wa kihistoria kwa Taifa Stars, ambao kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya AFCON kupitia mfumo wa timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu. Tanzania ilimaliza katika Kundi C lililokuwa na Nigeria, Tunisia na Uganda, ikikusanya sare mbili na kipigo kimoja, matokeo yaliyoitosha kuiweka kwenye orodha ya timu nne bora za nafasi ya tatu sambamba na Benin, Sudan na Msumbiji.

Kwa upande mwingine, Morocco, wenyeji wa mashindano haya, walimaliza kileleni mwa Kundi A baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare moja, wakikusanya jumla ya pointi saba. Rekodi hiyo inaifanya Morocco kuingia kwenye mchezo huu ikiwa na matumaini makubwa ya kuendelea na safari ya kutafuta taji lao la pili la AFCON tangu walipotwaa ubingwa mwaka 1976.

Historia ya kukutana: Morocco mbele kwa rekodi

Kwa mujibu wa rekodi za awali, timu hizi zimewahi kukutana mara nane katika michuano mbalimbali ikiwemo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026. Morocco imeshinda mechi saba kati ya hizo, huku Tanzania ikipata ushindi mmoja pekee, uliopatikana Machi 24, 2013, Taifa Stars ilipoifunga Morocco mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2014.

Katika ushindi huo wa kihistoria, Simon Msuva, Shomari Kapombe na Mbwana Samatta walikuwa sehemu ya kikosi, na baadhi yao bado wapo katika kikosi cha sasa, wakilenga kusaidia Taifa Stars kuvunja rekodi na kufuzu robo fainali ya AFCON kwa mara ya kwanza.

Presha kwa wenyeji, matumaini kwa Tanzania

Kimaendeleo na kwa majina ya wachezaji, Morocco inaingia kama favorite. Hata hivyo, presha kubwa ipo kwa wenyeji kutokana na matarajio ya mashabiki wao na ukosoaji unaoelekezwa kwa mbinu za kocha Walid Regragui, licha ya kikosi chake kuonyesha uimara kwenye hatua ya makundi.

Kwa upande wa Tanzania, kocha Miguel Gamondi ameisuka timu inayocheza kwa nidhamu ya hali ya juu, hususan katika ulinzi. Mfumo wa 5-4-1 uliotumika dhidi ya Tunisia uliifanya Stars kuwa timu ngumu kufungika, mechi hiyo ikimalizika kwa sare ya 1-1. Stars imeruhusu mabao manne pekee katika mechi tatu za makundi, ishara ya uimara wa safu ya nyuma.

Kikosi cha Taifa Stars vs Morocco leo

Kocha Miguel Gamondi amewapanga wachezaji wake kwa tahadhari kubwa, akianza na:

Kikosi cha kwanza:

  • Hussein Masalanga (GK)
  • Haji Mnoga
  • Mohamed Hussein
  • Dickson Job
  • Ibrahim Hamad
  • Bakari Mwamnyeto (C)
  • Novatus Miroshi
  • Alphonce Mabula
  • Feisal Salum
  • Selemani Mwalimu
  • Simon Msuva

Wachezaji wa akiba: Zuberi Foba, Pascal Msindo, Nickson Kibabage, Iddi Nado, Kibu Denis, Wilson Nangu, Khalidi Iddi, Lusajo Mwaikenda, Tarryn Allarakha, Yusuph Kagoma, Kelvin Nashon, Shomari Kapombe, Mbwana Samatta, Charles M’Mombwa.

Fuatilia Hapa Matokeo ya Tanzania Taifa Stars vs Morocco Leo 04/01/2026

Tanzania VS Morocco

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya AFCON 2025 Hatua Ya 16 Bora
  2. Tanzania Yafuzu 16 Bora AFCON Kwa Mara ya Kwanza
  3. Matokeo ya Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025
  4. Msimamo wa Kundi C La Tanzania AFCON 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo