Simba Day 2024 LIVE: Ubaya Ubwela, Mkapa Yafurika Mashabiki
Leo ni siku ya kihistoria kwa mashabiki wa Simba Sports Club wanapokusanyika kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, wakisherehekea Simba Day 2024 kwa shangwe na nderemo zisizo kifani. Ni siku ambayo wameipa jina la “Unyama Mwingi,” na hakika unyama huo unaonekana kwa jinsi mashabiki walivyojitokeza kwa maelfu, wakiwa wamevalia jezi nyekundu na nyeupe za timu yao pendwa.
Mashabiki wa Simba wamejitokeza kwa wingi, wakipamba uwanja na rangi za timu yao. Tangu alfajiri, maeneo ya kuingilia uwanja yalionekana na msururu wa mashabiki waliojaa furaha na matarajio makubwa. Video zilizorekodiwa zinaonesha umati mkubwa ukiwa umevalia jezi na bendera za Simba, huku nyimbo za hamasa zikiimbwa kwa sauti kubwa.
Burudani ya kutoka kwa wasanii nyota mbalimbali na madj wenye uwezo wa viwango vya kimataifa, wamekua chanzo kikubwa cha burudani katika Simba Day mwaka huu, na kuifanya kutia moto uwanjani. Ngoma za asili, na maonyesho ya kipekee yamewafanya mashabiki kucheza na kuimba kwa furaha. Ni wazi kuwa Simba imeweka juhudi kubwa kuhakikisha mashabiki wao wanapata burudani ya kiwango cha juua.
Moja ya matukio yaliokua yanasubiriwa kwa hamu kubwa ni utambulisho wa kikosi kipya cha Simba kitakachoshiriki katika michuano ya msimu wa 2024/25. Mashabiki wamekuwa na hamu ya kuona nyuso mpya zitakazovaa jezi ya Simba msimu huu, na utambulisho huu utaongeza msisimko zaidi kuelekea msimu mpya wa soka.
Angalia Hapa Simba Day 2024 LIVE
Angalia Picha za Matukio Kutoka Sherehe ya Simba Day 2024
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti