Matokeo ya Uganda Vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025

Matokeo ya Uganda Vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo kinashuka dimbani kuwakabili majirani zao Uganda katika mchezo wa pili wa Kundi C wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, mechi yenye uzito mkubwa kwa mustakabali wa timu zote mbili katika mashindano hayo. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Al-Barid, Rabat nchini Morocco, kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, huku ukirushwa mubashara kupitia Azam Sports 1 HD.

Taarifa Muhimu za Mchezo

  • Mchezo: Uganda vs Tanzania (Taifa Stars)
  • Tarehe: Leo, Jumamosi 27 Desemba 2025
  • Saa: 19:30 EAT (saa 2:30 usiku kwa saa za Tanzania)
  • Mashindano: AFCON 2025 – Hatua ya Makundi (Kundi C)
  • Uwanja: Al-Barid Stadium, Rabat – Morocco

Mchezo wa leo unakutanisha wapinzani wa muda mrefu kutoka Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya fainali za AFCON. Tanzania na Uganda zote zinaingia katika mchezo huu zikiwa hazina pointi, baada ya kupoteza mechi zao za kwanza. Taifa Stars ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria, huku Uganda ikikubali kipigo cha mabao 3-1 mbele ya Tunisia.

Kwa mujibu wa mfumo wa mashindano, timu 12 zitakazomaliza nafasi ya kwanza na ya pili katika makundi zitafuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora, huku timu nne bora zilizomaliza nafasi ya tatu zikiungana nazo. Hali hii inafanya ushindi wa leo kuwa muhimu zaidi kwa Tanzania na Uganda katika mbio za kuendelea na mashindano.

Historia ya Mikutano ya Tanzania na Uganda

Ingawa ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana kwenye fainali za AFCON, Tanzania na Uganda zimekutana mara 61 katika mashindano mbalimbali.

  • Uganda: Michezo 61, Ushindi 33, Sare 16, Vipigo 12
  • Tanzania: Michezo 61, Ushindi 12, Sare 16, Vipigo 33

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa katika mechi za kufuzu AFCON 2023, ambapo kila moja ilishinda ugenini kwa bao 1-0. Taifa Stars ilimaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo mbele ya Uganda na kufuzu fainali zilizofanyika Côte d’Ivoire.

Rivalry hii ilianza rasmi Septemba 8, 1964, Tanzania ilipoifunga Uganda mabao 3-0 kwenye Kombe la Afrika Mashariki. Ushindi mkubwa zaidi wa Uganda dhidi ya Stars ni ule wa mabao 5-0 katika CECAFA Cup mwaka 1991.

Matokeo ya Uganda Vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025

Fuatilia Hapa Matokeo ya Uganda Vs Tanzania Taifa Stars Leo 27/12/2025

UGANDA VS TANZANIA

Takwimu Muhimu – Uganda

Uganda inaingia katika mchezo huu ikiwa na rekodi ngumu katika fainali za AFCON. Kipigo dhidi ya Tunisia kilikuwa cha 17 katika mechi 24 walizocheza katika historia ya mashindano haya. Bao la Denis Omedi katika dakika za mwisho lilimaliza ukame wa dakika 376 bila kufunga bao AFCON.

Katika mechi hiyo, Uganda ilipata shuti moja tu lililoelekea langoni, likiwa ndilo lililozalisha bao. Khalid Aucho, nahodha wa timu, na Steven Mukwala wote wanacheza soka la kulipwa Tanzania, jambo linaloongeza mvuto wa pambano la leo.

Takwimu Muhimu – Tanzania Taifa Stars

Kwa upande wa Taifa Stars, kipigo cha 2-1 dhidi ya Nigeria kilikuwa mechi ya 10 kwa Tanzania katika historia ya fainali za AFCON. Licha ya kutopata ushindi katika mechi zake zote 10, Stars imefanikiwa kufunga bao katika michezo sita kati ya hiyo.

Charles M’Mombwa, aliyefunga bao pekee dhidi ya Nigeria, ameendelea kuwa mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji, akihusika na mabao matatu kati ya manne ya mwisho ya Tanzania katika mashindano yote. Kipa Zuberi Foba aling’ara kwa kuokoa mashuti manane dhidi ya Nigeria, akiwa miongoni mwa makipa waliofanya kazi kubwa zaidi katika raundi ya kwanza.

Akizungumza baada ya mchezo wa kwanza, Foba alisema:

“Kilichobaki tuombeane katika michezo ijayo tulisogeze Taifa pale tunapotaka kulisogeza. Kwa mimi naamini tunaweza kuvuka hatua ya makundi.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Makundi AFCON 2025
  2. Msimamo wa Kundi C La Tanzania AFCON 2025
  3. Matokeo ya Nigeria vs Tanzania Leo 23/12/2025 AFCON
  4. Kikosi cha Tanzania vs Nigeria Leo 23/12/2025 AFCON
  5. Ratiba ya Mechi za AFCON Leo 23/12/2025
  6. Bao la Dakika za Mwisho la Patson Daka Lainusuru Zambia Dhidi ya Mali, Mechi Ikiisha 1-1
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo