Matokeo ya Usaili TRA April 2025, Majina ya Waliofaulu Usaili TRA 2025

usaili TRA

Matoko ya Usaili TRA April 2025, Majina ya Waliofaulu Usaili TRA 2025

Matokeo ya Usaili TRA April 2025, Majina ya Waliofaulu Usaili TRA 2025 | Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Wa Oral na Vitendo TRA April 2025 | Orodha ya Waliopia Usaili wa Mchujo Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA

Dar es Salaam, Aprili 2, 2025 – Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kuwa matokeo ya usaili wa maandishi kwa waombaji kazi uliofanyika Machi 29 na 30, 2025, yatatolewa rasmi Aprili 25, 2025. Taarifa hii imetolewa na Mkurugenzi wa Usimamizi na Utawala wa Rasilimali Watu wa TRA, Moshi Kabengwe, ambaye alieleza kuwa matokeo yatatolewa mara baada ya kupokelewa kutoka kwa mshauri wa taaluma aliyesimamia zoezi hilo, ambaye anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake Aprili 23, 2025.

Matokeo ya Usaili TRA April 2025, Majina ya Waliofaulu Usaili TRA 2025

Ratiba ya Usaili wa Vitendo na Mahojiano

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya usaili wa maandishi, Mamlaka ya Mapato Tanzania imepanga kuanza hatua inayofuata ya usaili wa vitendo na mahojiano kwa waombaji waliopata mafanikio.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kabengwe:

  • Usaili wa Vitendo utafanyika kuanzia Mei 2 hadi 4, 2025, kwa kada za madereva na waandishi waendesha ofisi.
  • Usaili wa Mahojiano kwa kada nyingine zote utafanyika kuanzia Mei 7 hadi 9, 2025.

Ratiba rasmi ya usaili wa vitendo na mahojiano itatolewa kupitia tovuti ya TRA tarehe 29 Aprili, 2025. Waombaji wote wanashauriwa kufuatilia taarifa hiyo kwa karibu kupitia vyanzo rasmi.

Mafunzo Rasmi ya Ajira na Mwelekeo

Kwa waombaji watakaofaulu majaribio ya vitendo na mahojiano, TRA imetangaza kuwa:

Taarifa rasmi ya ufaulu zitatolewa tarehe 18 Mei, 2025.

Mafunzo elekezi kwa watumishi wapya yataanza tarehe 22 Mei hadi Juni 2, 2025.

Baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo, watumishi wapya wataanza kazi rasmi ndani ya Mamlaka.

Takwimu Muhimu Kuhusu Mchakato wa Usaili

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Moshi Kabengwe, mchakato wa usaili wa ajira mwaka 2025 umehusisha idadi kubwa ya waombaji kama ifuatavyo:

  • Jumla ya maombi 112,952 yalihesabiwa kuwa yamekidhi vigezo.
  • Maombi 71 ya nyongeza yalipokelewa kupitia rufaa, na kuifanya idadi ya jumla kuwa 113,023 kutoka kwa waombaji 86,314.
  • Watahiniwa 78,544 walishiriki katika usaili wa maandishi, sawa na asilimia 91 ya waombaji wote waliokidhi vigezo.
  • Waombaji 7,770 (asilimia 9) hawakufika kwenye usaili kutokana na sababu mbalimbali.

Kabengwe alisisitiza kuwa mchakato mzima wa ajira unatekelezwa kwa misingi ya uwazi, usawa, na kuzingatia sifa za kitaaluma, bila kujali hadhi ya mwombaji kijamii. Aidha, vituo vya usaili vilisambazwa katika mikoa minane pamoja na Zanzibar ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa waombaji kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Pakua Matoko ya Usaili TRA April 2025, Majina ya Waliofaulu Usaili TRA 2025

Mapendekezo ya Mhariri

  1. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025
  2. Majina Ya WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji 2025
  3. Usaili Jeshi la Zimamoto 2025 Kuanza Aprili 5 – 17, 2025
  4. Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Polisi 2025
  5. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA 2025 pdf
  6. Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Polisi 2025
  7. Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya Jeshi la Polisi Tanzania 2025
  8. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA Kutangazwa Machi 22, 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo