Matokeo ya Yanga VS Dodoma Jiji Leo 22/06/2025 | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Dodoma Jiji Ligi Kuu
Timu ya Wananchi, Yanga SC, leo tarehe 22 Juni 2025 inatarajiwa kushuka dimbani katika uwanja wa New Amaan, Zanzibar kuwakabili Dodoma Jiji FC katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Huu ni mchezo wa raundi ya 30 wa ligi, ukiwa ni wa mwisho kabla ya mtanange wa kiporo dhidi ya watani wa jadi Simba SC tarehe 25 Juni.
Kwa Yanga, huu si mchezo wa kawaida, bali ni fursa ya kujiweka sawa na kuimarisha nafasi yao ya kutetea ubingwa. Timu hiyo inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 76, ikiwa mbele ya Simba wenye pointi 75. Matokeo ya Yanga VS Dodoma Jiji Leo 22/06/2025 yatakuwa ya kihistoria kwa mashabiki na wadau wa soka, kwani yanaweza kufungua au kufunga mlango wa ubingwa wa msimu huu.
Mchezo huu umepangwa kuanza saa 10:00 jioni (16:00) na unatarajiwa kuvuta hisia za maelfu ya mashabiki wa soka nchini na nje ya mipaka. Kikosi rasmi cha Yanga kinatarajiwa kutangazwa saa 9:00 alasiri.
Kocha mkuu Miloud Hamdi anatarajiwa kuwaanzisha nyota wake tegemeo kama Prince Dube, Stephane Aziz Ki, Pacome Zouzoua na Clement Mzize ambao wote wamo kwenye mbio za tuzo ya mfungaji bora wa msimu. Kwa upande wa safu ya ulinzi, kipa Djigui Diarra atakuwa na jukumu la kuhakikisha clean sheet ya 17, ikiwa ni hatua muhimu ya kumkaribia Moussa Camara wa Simba aliye na 18.
Licha ya tayari kujihakikishia kubaki Ligi Kuu, wachezaji wa Dodoma Jiji hawajaingia kambini kwa mchezo huu kwa dharau. Winga wao Idd Kipagwile, ambaye amehusika katika mabao 11 msimu huu (mabao 7 na asisti 4), amesema wataingia uwanjani kwa heshima na dhamira ya kuhitimisha msimu kwa heshima, licha ya changamoto ya kuikabili timu ngumu kama Yanga.
Kipagwile amesisitiza kuwa licha ya kucheza bila presha ya kushuka daraja, wanahitaji heshima na watajitahidi kugawana pointi au hata kuvuna ushindi mbele ya mabingwa watetezi.
Matokeo ya Yanga VS Dodoma Jiji Leo 22/06/2025
Yanga Sc | VS | Dodoma Jiji |
Muktadha wa Msimu na Umuhimu wa Ushindi Leo
Msimu huu wa 2024/2025 umekuwa wa ushindani mkubwa, ukiwa umeweka rekodi mpya za mabao, penalti na ushindani wa mfungaji bora. Hadi kufikia leo, mechi 231 zimechezwa na mabao 544 kufungwa—rekodi inayovuka msimu uliopita wa mabao 517 katika mechi 240.
Yanga SC ikiwa na pointi 76 kabla ya mchezo huu, inahitaji ushindi dhidi ya Dodoma Jiji ili kujihakikishia nafasi ya kutwaa taji kwa mikono yao wenyewe. Ikumbukwe kuwa Simba pia wanacheza leo dhidi ya Kagera Sugar. Kushindwa kwa Yanga kuchukua pointi tatu kutamaanisha kwamba Simba wanaweza kuwapiku ikiwa wataibuka na ushindi katika mechi yao.
Mbio za Tuzo Binafsi na Rekodi za Msimu
- Ufungaji Bora: Prince Dube na Clement Mzize (Yanga) wako nyuma ya Jean Charles Ahoua wa Simba.
- Clean Sheets: Djigui Diarra (Yanga) anawania nafasi ya kwanza dhidi ya Camara wa Simba.
- Hat trick: Wachezaji wawili wa Yanga—Prince Dube na Aziz Ki—wameshatoa hat trick msimu huu.
- Asisti: Maxi Mpia Nzengeli na Pacome Zouzoua (Yanga) wanawania kuipiku rekodi ya Feisal Salum (Azam) mwenye asisti 13.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Yanga VS Dodoma Jiji Leo 22/06/2025
- Matokeo ya Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025
- Kikosi cha Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025
- Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?
- Yanga vs Dodoma Jiji Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?
- TFF Yafunga Rasmi Zoezi la Uchukuaji wa Fomu za Uongozi – Wagombea 25 Wajitokeza
- Tanzania Yashinda Ubingwa wa CECAFA Wanawake 2025 Kupitia Twiga Stars
- KMKM Mabingwa wa FA Cup Zanzibar 2025 Baada ya Ushindi wa 4-2 Dhidi ya Chipukizi
- Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Klabu ya Liverpool Yamwaga Mamilioni Kumnasa Florian Wirtz
- Viingilio Simba SC vs Kagera Sugar 22/06/2025
Leave a Reply