Matokeo ya Yanga vs KMC Leo 09/11/2025
Yanga SC leo itaingia kwenye Uwanja wa KMC Complex ikiwa na dhamira ya kupata ushindi muhimu utakaowarejesha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League). Mabingwa hao watetezi wanawavaa KMC FC katika mchezo utakaopigwa saa 10:00 Jioni, Jumapili 09 Novemba 2025, huku pande zote zikiwa na malengo tofauti msimu huu.
Yanga wanashuka dimbani wakiwa na alama 7 baada ya mechi 3, huku wakiwa bado hawajaruhusu bao lolote msimu huu wa ligi, na tayari wamefunga mabao matano. Kwa upande mwingine, KMC wanakuja kwenye mchezo huu wakiwa na alama 3 baada ya mechi 5, hali inayowafanya kukaa mkiani mwa msimamo na kuongeza shinikizo kwa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Marcio Maximo.
Kauli za Benchi la Ufundi – Yanga Wajiamini
Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Patrick Mabedi, amesema maandalizi ya mchezo huu yamekamilika na timu ina ari kubwa ya kuendelea na mwenendo wa matokeo chanya.
“Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa kesho, wachezaji wanajitoa na wanaendelea kupokea maelekezo kwa ubora. Tunatarajia kushinda,” alisema Mabedi.
Aliongeza pia msisitizo juu ya umuhimu wa kuheshimu kila mpinzani:
“Kila timu ina malengo yake, lazima tuuheshimu mchezo. Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tumejipanga kushinda,” alihitimisha.
Rekodi za Uso kwa Uso (H2H) – Yanga Wameutawala Michezo Iliopita
Takwimu zinaonyesha Yanga imekuwa na ubabe mkubwa dhidi ya KMC katika mechi za hivi karibuni:
| Tarehe | Mchezo | Matokeo |
|---|---|---|
| 14/02/2025 | KMC vs Yanga | 1-6 |
| 29/09/2024 | Yanga vs KMC | 1-0 |
| 17/02/2024 | KMC vs Yanga | 0-3 |
| 23/08/2023 | Yanga vs KMC | 5-0 |
| 22/02/2023 | KMC vs Yanga | 0-1 |
| 26/10/2022 | Yanga vs KMC | 1-0 |
| 19/03/2022 | Yanga vs KMC | 2-0 |
| 10/04/2021 | Yanga vs KMC | 1-1 |
| 25/10/2020 | KMC vs Yanga | 1-2 |
| 12/10/2020 | KMC vs Yanga | 1-0 |
| 02/12/2019 | Yanga vs KMC | 1-1 |
| 10/03/2019 | Yanga vs KMC | 2-1 |
| 25/10/2018 | KMC vs Yanga | 0-1 |
Fomu ya Hivi Karibuni – Yanga SC (Mechi 5 Zilizopita)
- 24/09/2025 – Yanga 3-0 Pamba Jiji
- 30/09/2025 – Mbeya City 0-0 Yanga
- 18/10/2025 – Silver Strikers 1-0 Yanga (CAF CL)
- 25/10/2025 – Yanga 2-0 Silver Strikers
- 28/10/2025 – Yanga 2-0 Mtibwa Sugar
Fomu ya Hivi Karibuni – KMC FC (Mechi 5 za Ligi)
- 17/09/2025 – KMC 1-0 Dodoma Jiji
- 23/09/2025 – KMC 0-1 Singida Black Stars
- 27/09/2025 – Tanzania Prisons 1-0 KMC
- 18/10/2025 – KMC 0-3 Mbeya City
- 25/10/2025 – Fountain Gate 1-0 KMC
Matokeo ya Yanga vs KMC Leo 09/11/2025
| Yanga Sc | VS | KMC Fc |
🏆 #nbcpremierleague
🆚 KMC FC (H)
🗓️ 09 November 2025
🏟️ KMC Complex
⏱️ 10:00 Jioni
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga vs KMC Leo 09/11/2025 Sasa Ngapi?
- Kikosi cha Simba vs JKT Tanzania Leo 08/11/2025
- Kikosi cha Yanga vs KMC Leo 09/11/2025
- Ratiba ya Ligi Kuu Wanawake Tanzania (TWPL) 2025/2026
- Droo ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
- Yanga Yaangukia Kundi B na Al Ahly Droo ya Makundi Klabu Bingwa 2025/2026
- Msimamo Kundi la Yanga Klabu Bingwa 2025/2026









Leave a Reply