Matokeo ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Pamaba Jiji
Mabingwa watetezi wa NBC Premier League (NBCPL), Yanga SC leo wanaanza rasmi kampeni yao ya kutetea taji la ligi kwa kuwakaribisha Pamba Jiji FC leo tarehe 24 Septemba 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Huu ni mchezo wa kwanza wa Wanajangwani msimu huu wa 2025/26 na unatarajiwa kutoa taswira ya mwelekeo wa mbio za ubingwa.
Yanga SC inashuka dimbani ikiwa na morali ya juu baada ya kupata ushindi mkubwa wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Wiliete SC ya Angola katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Aidha, kabla ya mchezo huu, Yanga pia iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC katika Ngao ya Jamii Septemba 16, jambo lililoongeza ari kwa kikosi cha Romain Folz.
Kwa upande wa Pamba Jiji, kikosi cha Francis Baraza kinaingia dimbani kikiwa kimetoka kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo FC kwenye Uwanja wa Majaliwa Septemba 18. Katika mchezo huo, Shaphan Siwa alifunga bao la kwanza kwa timu hiyo msimu huu dakika ya 19, kabla ya safu yao ya ulinzi kuruhusu goli la kusawazisha dakika ya 90+7.
Matokeo ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025
Matokeo kamili ya mchezo huu yataendelea kusasishwa hapa chini punde baada ya dakika 90 kumalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Yanga SC wanaingia uwanjani wakiwa na nafasi kubwa ya kuendeleza ubabe wao, lakini Pamba Jiji nao wanahitaji matokeo chanya ili kuimarisha nafasi yao msimu huu.
Yanga Sc | vs | Pamba Jiji |
- 🏆 #nbcpremierleague
- 🆚 Pamba Jiji FC
- 🗓️ 24 September 2025
- 🏟️ Benjamin Mkapa
- ⏱️ 1:00 Usiku
Mashabiki wanatarajia mchezo wenye ushindani kutokana na mbinu tofauti za makocha hawa wawili. Folz, ambaye ameanza msimu na matokeo mazuri ya kimataifa, atatafuta ushindi wa kwanza wa ligi ili kuendeleza rekodi ya Yanga ya kutopoteza michezo 20 mfululizo ya Ligi Kuu. Kwa upande mwingine, Baraza na vijana wake kutoka Mwanza wanalenga kuvunja mwiko wa kushindwa kila wanapokutana na Wanajangwani.
Kikosi cha Yanga SC Kinachotarajiwa Leo
Kocha Romain Folz anatarajiwa kuwatumia mastaa wake akiwemo kipa Djigui Diarra, mabeki Israel Mwenda na Dickson Job, pamoja na viungo na washambuliaji nyota kama Mohamed Doumbia, Clement Mzize, na Pacome Zouzoua. Wachezaji wa akiba ni pamoja na Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari na Mudathir Yahya.
Kikosi cha Pamba Jiji FC Kinachotarajiwa Kuanza Leo
Kwa upande mwingine, Kocha Francis Baraza anawaamini wachezaji wake akiwemo kipa Yona Amosi, mabeki Shassiri Nahimana na Abdoulaye Kunambi, huku safu ya ushambuliaji ikiwategemea James Mwashinga na Kelvin Nashon. Wachezaji wa akiba ni pamoja na Abdulmajid Mangalo, Michael Samamba na Najim Mussa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya NBC Premier league 2025/2026
- Serikali Yatoa Ufafanuzi Pamba Jiji Kufanya Mazoezi Gizani Uwanja wa Taifa
- Kikosi cha Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025
- Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Mechi za Leo 24/09/2025
- Fadlu Davids Atambulishwa Kama Kocha Mkuu wa Raja Casablanca ya Morocco
- Lamine Yamal Abeba Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka (Kopa Trophy)
Leave a Reply