Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo 25/06/2025

Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo 25/06/2025 | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Simba

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Ule mchezo wa kusisimua wa Kariakoo Dabi ambao ulikuwa ukiahirishwa mara kwa mara kutokana na sintofahamu baina ya Simba SC, Yanga SC na Bodi ya Ligi, hatimaye unachezwa leo tarehe 25 Juni 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 11 jioni.

Yanga SC ambao ni wenyeji wa mchezo huo, wataingia uwanjani wakihitaji pointi moja pekee ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya nne mfululizo. Kwa upande mwingine, Simba SC wanahitaji ushindi wa lazima ili kuvunja utawala huo na kutwaa taji lao la kwanza tangu msimu wa 2020/2021.

Hii si mechi ya kawaida. Ni mchezo wa ubingwa, unaobeba heshima, historia, na hatima ya msimu mzima wa 2024/2025. Ndiyo maana macho yote ya mashabiki wa soka Tanzania na Afrika Mashariki yapo kwenye Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo 25/06/2025.

Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kabla ya mechi hii muhimu ni kama ifuatavyo:

Pos Timu P W D L GF GA GD Pts
1 Young Africans 29 26 1 2 81 10 71 79
2 Simba 29 25 3 1 69 11 58 78
3 Azam FC 30 18 7 5 55 19 36 61
4 Singida Black Stars 30 17 6 7 45 26 19 57
5 Tabora 30 10 8 12 28 45 -17 38
6 JKT Tanzania 30 8 12 10 27 27 0 36
7 Mashujaa FC 30 8 11 11 29 33 -4 35
8 Coastal Union 30 8 11 11 26 31 -5 35
9 Namungo FC 30 9 8 13 28 36 -8 35
10 KMC 30 9 8 13 26 43 -17 35
11 Pamba 30 8 10 12 22 33 -11 34
12 Dodoma Jiji FC 30 9 7 14 31 49 -18 34
13 Tanzania Prisons 30 8 7 15 26 46 -20 31
14 Fountain Gate 30 8 6 16 32 57 -25 30
15 Kagera Sugar 30 5 8 17 22 41 -19 23
16 Kengold FC 30 3 7 20 22 62 -40 16

Kwa mantiki hiyo, sare tu inatosha kwa Yanga kutetea ubingwa, huku Simba wakilazimika kupata ushindi ili kuwapiku watani wao wa jadi. Tofauti hiyo ndogo ya pointi inafanya mchezo huu kuwa wa fainali isiyo rasmi ya Ligi Kuu ya NBC.

Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo 25/06/2025

Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo 25/06/2025 | Matokeo ya Yanga Leo vs Simba

YANGA SC VS SIMBA SC

Taariza Za Mechi Yanga Vs Simba Leo

  • 🏆 #nbcpremierleague
  • ⚽️ Young Africans SC🆚Simba SC
  • 📆 25.06.2025
  • 🏟 Benjamin Mkapa
  • 🕖 11:00 Jioni

Vikosi na Mbinu za Makocha

Yanga SC – Miloud Hamdi

Kocha Miloud Hamdi ameijenga Yanga kuwa timu yenye uwiano wa mashambulizi na ulinzi. Mfumo wake wa kawaida unahusisha mabeki wa pembeni Israël Mwenda na Chadrack Boka, huku mabeki wa kati wakiwa ni Dickson Job na Ibrahim Bacca.

Safu ya kiungo inaundwa na Khalid Aucho, Duke Abuya na Mudathir Yahya, huku mashambulizi yakiongozwa na Clement Mzize na winga hatari Pacome Zouzoua pamoja na Maxi Nzengeli.

Simba SC – Fadlu Davids

Kwa upande mwingine, Fadlu Davids wa Simba anatumia mfumo wa 4-2-3-1 unaobadilika kwa haraka kuwa 4-3-3. Ulinzi unaongozwa na Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Malone Fondoh, na Abdulrazak Hamza.

Kiungo wake cha ulinzi kinachezwa na Yusuph Kagoma na Fabrice Ngoma, huku nafasi ya namba 10 ikishikiliwa na Jean Charles Ahoua anayesimama nyuma ya washambuliaji Steven Mukwala au Leonel Ateba.

Vita ya Wachezaji – Mabao na Clean Sheets

Mechi ya Yanga VS Simba leo pia itaamua washindi wa tuzo binafsi:

  • Jean Charles Ahoua (Simba) ana mabao 16
  • Leonel Ateba (Simba), Steven Mukwala (Simba), Clement Mzize (Yanga), na Prince Dube (Yanga) wote wana mabao 13

Mshindi wa kiatu cha dhahabu atategemea matokeo ya leo. Aidha, upande wa makipa, Moussa Camara wa Simba ana clean sheets 19 huku Djigui Diarra wa Yanga akiwa na 16, hivyo Camara ameshashinda tuzo hiyo.

Rekodi ya Dabi na Changamoto za Uwanjani

Kwa zaidi ya miaka 48, hakuna mchezaji aliyefunga hat-trick kwenye Kariakoo Dabi, rekodi ya mwisho ikiwa ni ya Abdallah Kibadeni mwaka 1977. Wachezaji waliopo sasa wana nafasi ya kuvunja historia hiyo.

Katika safu ya ulinzi, Job na Bacca watajitahidi kumzuia Mukwala au Ateba, huku Malone na Hamza wakijaribu kuwazuia Mzize na Zouzoua. Katika winga, Elie Mpanzu na Kibu Denis wa Simba watapambana na mabeki wa Yanga, huku Maxi Nzengeli atakutana na Mohamed Hussein upande wa Simba.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vituo Vya Tiketi Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025
  2. Viingilio Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025
  3. Mechi ya Yanga vs Simba Kupigwa Chini ya Uangalizi wa Waamuzi Kutoka Misri
  4. Matokeo ya Yanga VS Dodoma Jiji Leo 22/06/2025
  5. Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
  6. Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC 22/06/2025
  7. TFF Yafunga Rasmi Zoezi la Uchukuaji wa Fomu za Uongozi – Wagombea 25 Wajitokeza
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo