Mechi ya Yanga Leo vs CBE SA 14/09/2024

Mechi ya Yanga Leo vs CBE SA 14/09/2024 | Matokeo ya Yanga Leo na Kikosi

Saa 9:00 alasiri leo, Jumamosi, Septemba 14, 2024, macho ya Watanzania yataelekezwa jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo mabingwa wa Tanzania, Yanga, watavaana na mabingwa wa Ethiopia, CBE SA, katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League 2024/2025).

  • 🔰Mechi ya Yanga VS CBE SA🔰
  • 🏆 #CAFCL
  • ⚽️ CBE SA🆚Young Africans SC
  • 📆 14.09.2024
  • 🏟 Azam Complex
  • 🕖 03:00PM

Fuatilia Hapa Matokeo CBE SA vs Yanga Leo 14 September 2024

Mechi ya Yanga Leo vs CBE SA 14/09/2024

Changamoto za Yanga Ugenini

Yanga watakuwa na kibarua kigumu mbele ya CBE, ambao wamepania kuandika historia mpya katika msimu wao wa kwanza kushiriki mashindano haya ya kifahari barani Afrika.

Kikosi cha Yanga kimetua Ethiopia kwa mafungu kutokana na wachezaji 14 kuwa kwenye majukumu ya timu za taifa ambapo walikua kupamania bendera za mataifa yao katika michuano ya kufuzu AFCON 2025, jambo linaloweza kuathiri muunganiko na maandalizi yao. Aidha, uchovu wa safari na kucheza ugenini ni changamoto nyingine ambazo wachezaji wa klabu ya Yanga watahitaji kuzishinda.

CBE: Timu Tishio Nyumbani

CBE ni timu inayomiliki mpira kwa ustadi mkubwa na kucheza soka la kushambulia, sawa na mtindo wa timu ya taifa ya Ethiopia. Wakiwa na faida ya kucheza mchezo huu nyumbani, CBE watataka kutumia udhaifu wowote utakao onyeshwa na kikosi cha Yanga kujipatia ushindi mnono kabla ya mchezo wa marudiano ukataochezwa Zanzibar.

Historia na Matarajio

Yanga haijawahi kushinda katika ardhi ya Ethiopia, na mara ya mwisho kucheza huko ilikuwa mwaka 2018 walipopoteza 1-0 dhidi ya Welayta Dicha. Hata hivyo, Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na uzoefu zaidi na kiu ya kufika makundi kwa msimu wa pili mfululizo.

CBE, kwa upande wao, wamepania kuandika historia kwa kufuzu hatua ya makundi katika msimu wao wa kwanza kushiriki Ligi ya Mabingwa. Wakiwa na kikosi kilichosheheni wachezaji wenye vipaji, CBE watakuwa wapinzani wagumu kwa Yanga.

Kwa kuzingatia falsafa za uchezaji zinazofanana za timu hizi mbili, mashabiki wa soka wanaweza kutarajia mchezo wa kusisimua utakaojaa mashambulizi kwa pande zote mbili. Uzoefu wa Yanga na hamasa ya CBE vinaweza kuufanya mchezo huu kuwa mgumu kutabiri.

Wapi Pa Kuutazama Mechi ya Yanga Leo vs CBE SA

Mchezo huu utarushwa moja kwa moja kupitia kisimbuzi cha Azam TV kuanzia saa 9:00 alasiri. Hakikisha umejiandaa mapema ili usikose pambano hili la kukata na shoka!

Angalia Hapa

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo