Michezo ya Yanga Sc Iliobaki Msimu wa 2024/2025

Michezo ya Yanga Sc Iliobaki Msimu wa 2024/2025

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC, wameweka wazi orodha ya michezo yao waliobakiza msimu huu wa 2024/2025 huku ikithibitika kuwa wamebakiza jumla ya michezo mitatu pekee.

Mechi mbili kati ya hizo ni za Ligi Kuu, huku mchezo mmoja ukiwa ni fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB. Taarifa hii imeibua mjadala mpana miongoni mwa mashabiki wa soka nchini, hasa baada ya Yanga kuendelea kusimamia msimamo wao wa kutoshiriki mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba SC, uliopangwa kufanyika tarehe 15 Juni 2025.

Yanga vs Tanzania Prisons

Kwa mujibu wa ratiba rasmi iliyotolewa na klabu hiyo, Yanga SC inatarajiwa kushuka dimbani kwa mara ya kwanza mwezi huu tarehe 18 Juni 2025 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa ugenini. Mchezo huo wa Ligi Kuu unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, na utakuwa ni nafasi muhimu kwa Wananchi kuendeleza ubabe wao katika mbio za kutetea taji lao.

Yanga SC Dhidi ya Dodoma Jiji FC

Baada ya hapo, mnamo tarehe 22 Juni 2025, Yanga SC itawakaribisha Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu. Mechi hii itakuwa ya mwisho kwa Yanga katika ligi kwa msimu huu, na mashabiki wanatarajia kuona kikosi hicho kikimaliza kwa kishindo, hasa kutokana na kiwango bora kilichoonyeshwa msimu mzima.

Yanga Sc dhidi ya Singida Big Stars

Mechi ya tatu na ya mwisho kwenye ratiba yao ni fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Singida Big Stars. Hadi sasa tarehe kamili ya mchezo huo haijatangazwa rasmi, lakini mechi hiyo inabeba uzito mkubwa kwani ni nafasi ya Yanga SC kuongeza taji jingine katika kabati lao la mafanikio msimu huu.

Michezo ya Yanga Sc Iliobaki Msimu wa 2024/2025

Kutokana na hali ya sasa, mashabiki wa soka nchini wanashuhudia kipindi cha mvutano wa kiusimamizi na kisiasa ndani ya soka la Tanzania, hasa kufuatia uamuzi wa Yanga kugomea mechi ya derby dhidi ya Simba SC. Hali hiyo imeacha sintofahamu kubwa na kuchochea mijadala kuhusu mustakabali wa soka la ushindani na nidhamu ya klabu zinazoshiriki Ligi Kuu.

Huku kila mechi iliyobaki ikiwa na umuhimu mkubwa, macho yote yataelekezwa kwa Yanga SC kuona kama watafanikiwa kumaliza msimu wakiwa na ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na taji la Kombe la Shirikisho.

Kocha mkuu pamoja na wachezaji wake wanaonekana kuwa na ari kubwa ya kuhakikisha historia inaandikwa upya, na mashabiki wana matumaini makubwa ya kuona timu yao ikitimiza malengo yote ya msimu huu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa kambini Kuelekea COSAFA na Mechi ya Kirafiki
  2. Dembélé Amechaguliwa Kuwa Mchezaji Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/25
  3. Siku ya Kuripoti Chuo cha Polisi Moshi 2025 kwa Vijana Waliochaguliwa
  4. Wafungaji Bora Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
  5. Fiston Mayele Ndie Mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2024/2025
  6. Washindi Tuzo Za Baraza La Michezo Tanzania BMT 2024
  7. Pyramids Yabeba Ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika 2024/2025 kwa Mara ya Kwanza Kihistoria
  8. Wachezaji wa Simba Walioitwa Kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa June 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo