Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (NSSF Balance Check)

Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (NSSF Balance Check)

Neno NSSF limetokana na maneno ya kingereza “National Social Security Fund” ambayo kwa kiswahili ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii. NSSF ni taasisi ya serikali ya Tanzania inayohusika na ukusanyaji, uwekezaji, na usambazaji wa michango ya wafanyakazi ili kuhakikisha maisha bora baada ya kustaafu. Ni muhimu kwa kila mfanyakazi kufahamu salio lake ili kupanga mustakabali wake kifedha.

Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (NSSF Balance Check)

Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (NSSF Balance Check)

Kwa wale wanaotaka kuangalia salio lao la NSSF kwa kutumia simu, kuna njia rahisi na ya haraka ya kufanya hivyo. Unachohitaji ni kuwa na simu yako yenye mtandao wa Tigo au Vodacom, na kufuata hatua zifuatazo:

Kuangalia Salio la Akaunti ya NSSF Kwa Njia Ya SMS

  1. Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
  2. Tuma ujumbe wenye neno “NSSF Balance” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama wa NSSF. Mfano: NSSF Balance 123456789.
  3. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.

Kupata Taarifa ya Statement ya Akaunti ya NSSF Kwa Njia Ya SMS

  1. Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
  2. Tuma ujumbe wenye neno “NSSF Statement” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama wa NSSF. Mfano: NSSF Statement 123456789.
  3. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.

Jinsi ya Kuangalia Salio La NSSF WhatsApp

  1. Hifadhi namba 0756 140 140 kwenye simu yako.
  2. Fungua WhatsApp na tuma ujumbe “Hello” au “Habari”.
  3. Fuata maelekezo ili kuangalia salio lako (“Balance”) au taarifa za michango (“Statement”)

Jinsi ya Kuangalia Salio la NSSF kwa Programu ya Simu Janja

  1. Pakua programu ya “NSSF Taarifa” kutoka Google Play Store.
  2. Ingia kwa kutumia maelezo yako ya NSSF.
  3. Angalia salio lako, michango, na taarifa nyingine muhimu.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia

  • Salio unalopokea kwa njia ya simu linaweza kuwa tofauti kidogo na lile utakalopewa moja kwa moja kwenye ofisi za NSSF. Hii ni kwa sababu kunaweza kuwa na mabadiliko madogo ambayo hayajaingizwa kwenye mfumo wa simu bado.
  • Njia Nyingine: Ili kupata taarifa kamili na sahihi zaidi, tembelea ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe.

Mawasiliano Zaidi na NSSF

Mawasiliano Zaidi na NSSF

Ikiwa unahitaji maelezo zaidi au msaada, unaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja wa NSSF kwa kutumia mawasiliano yafuatayo:

  • Barua pepe: [email protected]
  • Simu: 0 (75) 6140140 | 0800116773 | (255) (22) 2200037
  • Anwani: National Social Security Fund, P.O.Box 1322, Benjamin Mkapa Pension Towers, Azikiwe St, Dar Es Salaam, Tanzania.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Jinsi Ya Kuhakiki Bima Ya Gari (Car Insurance Validity Check In Tanzania)
  2. Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Tanzania
  3. Jinsi ya Kujiunga Vifurushi Simba Bando Vodacom
  4. Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2024
  5. eRITA Portal: Uhakiki wa Cheti cha Kuzaliwa 2024 (Njia Rahisi)
  6. Jinsi Ya kukata Tiketi Ya Treni Online (eticketing.trc.co.tz) 2024
  7. Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2024
  8. Jinsi ya Kuangalia Namba ya NIDA Online 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo