Mnyama Akusanya Pointi Zote Tatu Dhidi ya Wajelajela

Mnyama Akusanya Pointi Zote Tatu Dhidi ya Wajelajela

Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/2026 iliendelea katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambapo Simba SC waliingia dimbani wakisaka pointi tatu muhimu. Mnyama alitimiza lengo hilo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika dakika ya 18, Seleman Mwalimu aliifungia Simba bao la kwanza kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu. Simba waliendelea kudhibiti mchezo na kuongeza bao la pili dakika ya 45+1 kwa penalti iliyofungwa na Rushine De Reuck.

FT: Tanzania Prisons 0-2 Simba SC

⚽ 18’ Seleman Mwalimu
⚽ 45+1’ Rushine De Reuck (P)

Mnyama Akusanya Pointi Zote Tatu Dhidi ya Wajelajela

Kwa ushindi huo, Simba wanaendelea kupanda kwenye msimamo wa ligi wakiwa alama tatu nyuma ya Young Africans walio nafasi ya nne, huku Yanga wakiwa alama tatu nyuma ya vinara wa muda JKT Tanzania. Timu zote mbili za Dar es Salaam zina michezo kadhaa mkononi.

Simba sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye michezo ijayo ya ligi huku ushindani wa kileleni ukiendelea kushika kasi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Namungo FC vs Yanga Sc Leo 22/02/2026 Saa Ngapi?
  2. Ratiba ya Mechi za Leo 22/02/2026 Ligi Kuu ya NBC
  3. Mbio za Ubingwa EPL Zapamba Moto Baada ya Arsenal Kudondosha Pointi Dhidi ya Wolves
  4. Barcelona Yatakiwa Kulipa Pauni 26M Kumng’oa Rashford Manchester United
  5. Serikali Yaidhinisha Rasmi Marekebisho ya Katiba ya Simba SC Kupitia BMT
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo