Morocco VS Tanzania Leo 04/01/2026 Saa Ngapi?

Morocco VS Tanzania Leo 04/01/2026 Saa Ngapi?

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania, Taifa Stars, leo itakuwa katika dimba la Prince Moulay Abdellah, jijini Rabat, ikicheza mechi ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 dhidi ya wenyeji wa mashindano hayo, Morocco.

Mechi hii inatarajiwa kuchezwa leo Jumapili tarehe 04 Januari 2026 kuanzia saa 1:00 usiku, kwa saa za Afrika Mashariki, na imebeba uzito mkubwa kwa historia ya soka la Tanzania.

Morocco VS Tanzania Leo 04/01/2026 Saa Ngapi?

Umuhimu wa Mechi Hii kwa Taifa Stars

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwenye michuano ya AFCON, Taifa Stars imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika Kundi C lililokuwa na Nigeria, Tunisia na Uganda. Stars iliingia hatua hii kupitia kundi la washindwa bora, likiwa sambamba na timu za Benin, Sudan na Msumbiji.

Hatua hii inaifanya mechi ya Morocco VS Tanzania leo 04/01/2026 kuwa ya kihistoria, kwani Stars inatafuta kuvuka hatua ya mtoano na kutinga robo fainali ya AFCON kwa mara ya kwanza, mafanikio ambayo hayajawahi kupatikana kwenye AFCON, japokuwa Tanzania iliwahi kufika hatua hiyo kwenye CHAN 2024.

Morocco: Wenyeji Wenye Presha Kubwa

Morocco inaingia kwenye mechi hii ikiwa na rekodi nzuri, baada ya kumaliza kinara wa Kundi A kwa pointi saba, ikishinda mechi mbili na kutoka sare moja. Hata hivyo, pamoja na ubora wao, presha kubwa ipo upande wa wenyeji, ambao wamekuwa wakisubiri taji la AFCON tangu walipolitwaa mwaka 1976, na kulikosa tena katika fainali ya mwaka 2004.

Kocha wa Morocco, Walid Regragui, amekumbana na ukosoaji kutoka kwa wadau mbalimbali licha ya matokeo mazuri, jambo linaloongeza mzigo wa ushindi katika mechi ya leo dhidi ya Tanzania.

Historia ya Michezo ya Morocco VS Tanzania

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, timu hizi zimewahi kukutana mara nane kabla ya mechi ya leo, huku Morocco ikishinda mechi saba na Tanzania kushinda mara moja pekee. Ushindi pekee wa Taifa Stars dhidi ya Morocco ulitokea Machi 24, 2013, katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2014, ambapo Tanzania ilishinda 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika kikosi cha sasa cha Taifa Stars, wapo wachezaji watatu waliokuwepo kwenye ushindi huo wa kihistoria Mbwana Samatta, Simon Msuva na Shomari Kapombe ambao wanatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika pambano la leo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya AFCON 2025 Hatua Ya 16 Bora
  2. Tanzania Yafuzu 16 Bora AFCON Kwa Mara ya Kwanza
  3. Matokeo ya Tanzania vs Tunisia Leo 30/12/2025
  4. Msimamo wa Kundi C La Tanzania AFCON 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo