Mshambuliaji Clement Mzize Asaini Kuendelea na Yanga Hadi 2027
Mabosi wa Klabu ya Yanga SC wamethibitisha rasmi kuwa mshambuliaji wao hatari, Clement Mzize, ataendelea kusalia katika kikosi cha Jangwani hadi mwaka 2027. Uamuzi huo umefuta tetesi zote zilizokuwa zikimhusisha mchezaji huyo na kuondoka klabuni hapo kuelekea vilabu vya nje ya nchi. Kwa muda mrefu, Mzize alikuwa akihusishwa na miamba ya Afrika Kaskazini ikiwemo Esperance Sportive de Tunisia na Al Masry ya Misri. Hata hivyo, taarifa rasmi kutoka Yanga imethibitisha kuwa nyota huyo ataendelea kuwatumikia Wananchi kwa misimu miwili ijayo, akibaki kuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Clement Mzize bado ana mkataba wa muda mrefu na Yanga SC unaomfunga klabuni hadi mwaka 2027. Hii inamaanisha mashabiki wa Wananchi wataendelea kumuona akikipiga katika msimu wa 2025/2026 na 2026/2027.
Uwepo wa Mzize ndani ya kikosi unaongeza nguvu kubwa safu ya ushambuliaji ya Yanga, hasa ikizingatiwa kiwango chake cha ufungaji katika misimu ya hivi karibuni.
Takwimu za Kiwango cha Juu
Msimu uliopita wa 2024/2025, Clement Mzize alidhihirisha ubora wake akiwa kinara wa mabao wa klabu baada ya kufunga mabao 14 na kutoa asisti sita katika mechi zote 30 alizocheza. Ufanisi huo ulimfanya kuwa miongoni mwa washambuliaji bora wazawa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Safari yake ndani ya Yanga SC imekuwa ya mafanikio tangu alipopandishwa kutoka timu ya vijana mwaka 2022/2023. Katika msimu huo wa kwanza, alifunga mabao matano na kutoa asisti moja, akichangia moja kwa moja kwenye kutwaa ubingwa wa ligi. Msimu wa pili (2023/2024) aliongeza makali yake kwa kufunga mabao sita na kutoa asisti saba, huku akiwasaidia Wananchi kufanikisha mafanikio zaidi.
Mbali na ligi kuu, Mzize pia aling’ara kwenye Kombe la Shirikisho msimu wa 2023/2024 baada ya kufunga mabao matano katika michezo sita, ikiwemo hat-trick moja, na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Opah Clement Atambulishwa Rasmi SD Eibar ya Hispania
- Yanga SC Kucheza Dhidi ya Bandari FC Siku ya Wiki ya Mwananchi
- Morocco Yatinga Fainali ya CHAN Baada ya Kuifunga Senegal kwa Penalti
- Madagascar Kukipiga Dhidi ya Morocco Fainali ya CHAN 2025
- Simba SC Yasogeza Tarehe ya Uzinduzi wa Jezi Mpya 2025/2026
- Viingilio Simba Day 2025
- Ligi Kuu Zanzibar ZPL 2025/2026 kuanza Septemba 20
- Jezi Mpya za Yanga 2025/2026 | Picha za Jezi Mpya za Yanga
Leave a Reply