Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025

Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025

Jeshi la Uhamiaji Tanzania, kupitia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji na kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, limetangaza rasmi Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025.

Tangazo hili linalenga kuwaajiri vijana wa Kitanzania wenye sifa stahiki ili kujaza nafasi za Konstebo wa Uhamiaji, nafasi ambazo zinatoa fursa ya kuhudumia Taifa kupitia Idara ya Uhamiaji katika maeneo mbalimbali nchini.

Tangazo hili ni miongoni mwa matangazo muhimu ya ajira Serikalini kwa mwezi Desemba 2025, likiwa linatoa mwelekeo wazi kuhusu sifa za waombaji, vigezo vya kipaumbele, namna ya kuwasilisha maombi pamoja na tahadhari muhimu kwa waombaji wote.

Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025

Sifa za Mwombaji wa Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025

Kwa mujibu wa tangazo rasmi, waombaji wote wa Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025 wanatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:

  • Awe ni raia wa Tanzania.
  • Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na taasisi yoyote ya Serikali.
  • Awe na cheti halali cha kuzaliwa.
  • Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.
  • Awe na afya njema ya mwili na akili.
  • Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.
  • Asiwe na kumbukumbu au taarifa zozote za kuhusika katika vitendo vya uhalifu au jinai.
  • Asiwe na alama au michoro (tattoo) yoyote mwilini.
  • Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto.
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya kijeshi ya Uhamiaji.
  • Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote nchini Tanzania.
  • Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshaji wa zoezi la ajira.

Vigezo vya Umri na Kiwango cha Elimu

Kwa upande wa umri na elimu, Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025 zimegawanywa kama ifuatavyo:

  • Mwombaji mwenye elimu ya Kidato cha Nne anatakiwa awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu na awe na umri kati ya miaka 18 hadi 22.
  • Mwombaji mwenye Astashahada au Stashahada anatakiwa awe na umri wa miaka 18 hadi 25.
  • Mwombaji mwenye elimu ya Shahada au Stashahada ya Juu anatakiwa awe na umri wa miaka 18 hadi 30.

Maombi Yatakayopata Kipaumbele

Idara ya Uhamiaji imesisitiza kuwa kipaumbele kitatolewa kwa waombaji wenye elimu ya Astashahada, Stashahada, Shahada au Stashahada ya Juu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, hasa katika fani zifuatazo:

  • Lugha za Kimataifa
  • Utawala
  • Sheria
  • Uhusiano
  • TEHAMA, ikijumuisha Cyber Security, Database Developer, System Developer, Artificial Intelligence na Machine Learning
  • Masijala
  • Ukatibu Mahsusi
  • Uhasibu
  • Ununuzi na Ugavi (waliosajiliwa na Bodi husika)
  • Takwimu
  • Uchumi
  • Umeme
  • Ufundi wa AC
  • Brass Band
  • Saikolojia (Psychology)
  • Mpiga chapa (Printer)

Aidha, waombaji wenye ujuzi wa ufundi wa magari na udereva nao watapewa kipaumbele maalum katika zoezi hili la Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025.

Namna ya Kutuma Maombi ya Ajira Uhamiaji

Maombi yote ya Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025 yatawasilishwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti rasmi ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni www.immigration.go.tz.

Dirisha la maombi litafunguliwa kuanzia tarehe 29 Desemba 2025.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11 Januari 2026.

Wakati wa kuwasilisha maombi, mwombaji anatakiwa kupakia nyaraka zifuatazo katika mfumo wa PDF, ambapo kila nyaraka moja isizidi ukubwa wa 300KB:

  • Picha ya pasipoti ya hivi karibuni (jpg/png) isiyozidi 300KB.
  • Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono.
  • Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa waliopo makambini JKT/JKU wawe na barua kutoka kwa Mkuu wa Kambi.
  • Cheti cha kuzaliwa.
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA.
  • Namba za mtihani (Index Numbers) za Kidato cha Nne na Kidato cha Sita.
  • Namba ya utambuzi wa cheti cha Astashahada, Stashahada au Shahada/Stashahada ya Juu inayotambuliwa na TCU au NACTVET.
  • Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi.
  • Wasifu binafsi wa mwombaji (CV).

Kwa changamoto au maswali yanayohusiana na maombi ya Nafasi Mpya Za Kazi Uhamiaji December 2025, waombaji wanashauriwa kuwasiliana kupitia barua pepe: [email protected]

Mapendekezo ya Mhariri

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo