Viingilio Mechi ya Vital O FC Vs Yanga Klabu Bingwa 17/08/2024
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2023/2024, Yanga SC, wanajiandaa kuanza kampeni yao mpya katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) ambapo watakutana na timu ya Vital’O FC kutoka Burundi.
Mchezo huu wa kwanza umepangwa kutimua vumbi katika dimba la Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, mnamo Agosti 17, 2024. Mashabiki wa soka wanaotarajia kushuhudia mechi hii wana kila sababu ya kuwa uwanjani kwani inatarajiwa kuwa mtanange wa kukata na shoka, ambapo Yanga itaanza safari yake ya kusaka taji la kifahari barani Afrika.
Mechi hii itakuwa ni ya ufunguzi kwa Yanga SC katika msimu mpya wa michuano ya CAF, na itawapa nafasi ya kuonyesha umahiri wao baada ya msimu mzuri wa ligi ya ndani. Mashabiki na wapenzi wa soka wanaotaka kushuhudia mchezo huu live uwanjani wanapaswa kuhakikisha wanapata tiketi mapema, kwani viingilio vimepangwa ili kutoa nafasi kwa kila mmoja kufurahia burudani hii.
Hivi apa Viingilio vya Mechi ya Vital O FC Vs Yanga
- VIP A: Tsh 50,000
- VIP B: Tsh 30,000
- Mzunguko: Tsh 10,000
Mapendekezo ya Mhariri:
- Gamondi Apania Kumaliza Kazi Mapema Dhidi ya Vital’O
- Yanga SC Yaibua Matumaini ya Kufika Nusu Fainali CAF
- Singida Black Stars Tayari Kuivaa Kengold FC Katika Ligi ya NBC
- Awesu Kurudi KMC Baada ya Uamuzi wa Kamati ya Sheria ya TFF
- Mfalme Mpya Madrid, Mbappé Afunga Katika Mechi ya Kwanza
- Janga la Majeruhi Laendelea Kuiandama Azam FC
Weka Komenti