Nafasi za Kazi Jeshi la Zimamoto November 2025

Nafasi za Kazi Jeshi la Zimamoto November 2025

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetangaza nafasi mpya za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia cheti cha kidato cha nne hadi viwango vya kitaaluma katika fani mbalimbali. Tangazo hilo limetolewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John W. Masunga, likieleza kuwa ajira hizo ni kwa ngazi ya Konstebo na zinatolewa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya sheria husika za utumishi wa umma.

Tangazo hili linawahusu waombaji wanaokidhi sifa maalum za kiafya, kijamii, kitaaluma na kitabia, huku likiainisha utaratibu rasmi wa kuwasilisha maombi kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Nafasi za Kazi Jeshi la Zimamoto November 2025

Sifa za Mwombaji – Elimu ya Kidato cha Nne

Waombaji wa ngazi ya kidato cha nne wanapaswa kutimiza masharti yafuatayo:

  • Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
  • Awe na Kitambulisho cha Taifa au NIDA Number
  • Awe na afya njema kimwili na kiakili
  • Asiwe na rekodi yoyote ya uhalifu
  • Awe hajaoa au kuolewa
  • Asiwe na alama za michoro (tattoos)
  • Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
  • Awe hajawahi kuajiriwa serikalini
  • Awe na urefu usiopungua futi 5.7 (wanaume) na futi 5.4 (wanawake)
  • Awe tayari kushiriki hatua zote za usaili endapo ataitwa
  • Awe tayari kufanya kazi popote atakapopangiwa baada ya mafunzo
  • Umri uwe kati ya miaka 18 hadi 25

Ajira kwa Waliohitimu Kidato cha Nne au Sita (Ngazi ya Ufundi na Ujuzi)

Jeshi la zimamoto limetangaza nafasi kwa fani mbalimbali, ikijumuisha:

  1. Madereva wa magari makubwa
  2. Wauguzi ngazi ya Stashahada
  3. Taaluma za Zimamoto na Uokoaji
  4. Matabibu ngazi ya Stashahada
  5. Mafundi mchundo wa magari
  6. Wazamiaji na waogeleaji
  7. Wanamichezo
  8. Brass band
  9. Waandishi wa waendesha ofisi
  10. TEHAMA ngazi ya Stashahada
  11. Mafundi umeme na ndege ngazi ya Stashahada

Sifa za Mwombaji – Ngazi hizi zinahitaji:

a) Kutimiza sifa zote za Aya ya 1 (a hadi l)
b) Umri kati ya miaka 18 hadi 28
c) Wazamiaji na waogeleaji kufanyiwa uhakiki wa vitendo
d) Madereva kuwa na leseni daraja E na watakaofika kwenye usaili kufanyiwa uhakiki wa vitendo

Elimu ya Shahada

Nafasi zinapatikana kwa wahitimu wa shahada katika fani zifuatazo:

  • Uhandisi Bahari
  • TEHAMA
  • Uhandisi wa Ndege
  • Uwakadiriaji Majenzi (QS)
  • Sheria (waliomaliza shule ya sheria na kufuzu mafunzo ya vitendo)
  • Mafuta na gesi
  • Uhandisi ujenzi
  • Uhandisi mitambo
  • Uhandisi umeme

Sifa za Mwombaji – Shahada:

  • Kutimiza masharti yote ya Aya ya 1 (a hadi l)
  • Umri kuanzia miaka 18 hadi 28

Jinsi ya Kutuma Maombi Nafasi za Kazi Jeshi la Zimamoto November 2025

Waombaji wanapaswa kuwasilisha maombi kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia:
➡️ https://ajira.zimamoto.go.tz

Mwisho wa kutuma maombi: 03 Desemba 2025

Waombaji watahitajika kupakia nyaraka zifuatazo kwenye mfumo:

a) Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono, ikielekezwa kwa:

Kamishna Jenerali,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
1 Mtaa wa Zimamoto,
S.L.P 1509,
41102 DODOMA

b) Fomu ya uthibitisho wa afya njema kutoka kwa mganga wa serikali
c) Nakalahalisi au namba ya Kitambulisho cha NIDA
d) Namba za mtihani wa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita
e) Vyeti vya taaluma kutoka vyuo vinavyotambulika na serikali (Astashahada, Stashahada, Shahada)
f) Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa kupitia mfumo wa NaPA

Maelekezo Muhimu ya Kuzingatia

  • Nyaraka zilizothibitishwa nje ya masharti yaliyotajwa hazitakubaliwa
  • Maombi ya posta, mkono au barua pepe hayatapokelewa
  • Waombaji waandike namba za simu kwenye barua ya maombi
  • Mtu atakayewasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria
  • Waombaji wote watapimwa tena afya na akili wakifika chuoni

Tangazo limetolewa rasmi tarehe 19 Novemba 2025 na kusainiwa na:

John W. Masunga
KAMISHNA JENERALI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Bofya Hapa Kupakua Tangazo Rasmi

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  2. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE)
  3. Kidato cha Nne Kuanza Mitihani ya Taifa Kesho November 17 2025
  4. NECTA Standard Seven Results 2025 Released: 81.8% of Candidates Pass the PSLE Examination
  5. Tarehe Mpya za Kufunguliwa Vyuo 2025/2026 Zatangazwa na Wizara ya Elimu
  6. NECTA Yatangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2025 – Asilimia 81.80 Wamefaulu Nchini
  7. Mambo 5 ya Muhimu Kujua Wakati Wa Kusubiri Kutangazwa kwa Matokeo ya Darasa la Saba 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo