Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza ratiba ya mtihani wa Taifa kidato cha nne 2024/2025, utakaofanyika kuanzia tarehe 11 Novemba hadi 29 Novemba 2024. Mtihani huu ni muhimu sana katika mfumo wa elimu wa Tanzania, kwani ndio unaotumika kutathmini kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne na kuamua hatua zao zinazofuata katika masomo yao.
Ratiba hii inatoa mwongozo kamili wa tarehe, siku, na muda wa kila somo litakalofanyiwa mtihani. Aidha, inajumuisha maelekezo muhimu kwa wanafunzi, wazazi/walezi, na walimu kuhusu taratibu za mtihani na mambo mengine muhimu yanayohitaji kuzingatiwa.
Mitihani itahusisha masomo ya lazima na ya hiari, ikiwa ni pamoja na Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, Jiografia, Fizikia, Kemia, Baiolojia, na mengine mengi. Pia, kutakuwa na mitihani ya vitendo kwa baadhi ya masomo kama vile Baiolojia, Fizikia, na Kemia.
Katika ratiba hii, NECTA imesisitiza kuwa mitihani itaendelea kama ilivyopangwa hata kama siku ya mtihani itaangukia kwenye sikukuu. Aidha, wanafunzi wametakiwa kufika vituoni kwa wakati na kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa mitihani.
Ratiba ya Mtihani wa Taifa Kidato cha Nne 2024/2025
Mtihani wa Kidato cha Nne kwa mwaka wa masomo 2024 utafanyika kuanzia tarehe 11 Novemba hadi tarehe 29 Novemba 2024. Mitihani ya vitendo itaanza mapema tarehe 14 Novemba 2024. Ratiba ya mtihani huu imepangwa kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata fursa ya kufanya mtihani kwa haki na usawa.
Kama wewe ni mzazi, mlezi au mwalimu wa wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari, kusoma na kuelewa ratiba ya mtihani kidato cha nne ni muhimu sana. Hii itakusaidia kuhakikisha kuwa mwanafunzi anafahamu tarehe na siku za mitihani ya kila somo, na hivyo kuwawezesha kupanga muda wao wa kusoma vyema.
Kupitia ratiba hii, utaweza kuona ni lini mitihani ya vitendo itafanyika na kuhakikisha kuwa mwanafunzi amejiandaa ipasavyo. Vilevile, ratiba hii itakusaidia kuwa na ufahamu kuhusu muda wa mitihani na maelekezo mengine muhimu kutoka NECTA.
Hii Apa Ratiba ya Mtihani wa Taifa Kidato cha Nne 2024/2025
Ratiba kamili ya mitihani ni kama inavyo onekana katika picha ifuatayo:
Pakua PDF ya Ratiba ya Mtihani wa Taifa Kidato cha Nne 2024/2025 Hapa
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti