Nafasi Za Kazi Takukuru PCCB April 2026

Nafasi Za Kazi Takukuru PCCB April 2026

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza rasmi nafasi mpya za ajira kwa Watanzania wenye sifa stahiki, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo katika ngazi ya wilaya kote Tanzania Bara.

Tangazo hilo, lililochapishwa tarehe 11 Aprili 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, linatoa fursa kwa wataalamu na wahitimu wa kada mbalimbali kujiunga na taasisi inayosimamia mapambano dhidi ya rushwa nchini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jumla ya nafasi 500 zimetangazwa, zikigawanywa katika kada mbili kuu: Afisa Uchunguzi na Mchunguzi Msaidizi.

Nafasi Za Kazi Takukuru PCCB April 2026

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa PCCB

TAKUKURU imetangaza nafasi katika makundi yafuatayo:

  • Afisa Uchunguzi – Nafasi 250
  • Mchunguzi Msaidizi – Nafasi 250

Nafasi hizi zinalenga kuongeza nguvu kazi katika ofisi za wilaya, ili kuboresha ufanisi wa uchunguzi na utekelezaji wa majukumu ya taasisi.

Sifa za Afisa Uchunguzi (Nafasi 250)

Kwa nafasi ya Afisa Uchunguzi, waombaji wanatakiwa kuwa na shahada ya kwanza kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani mbalimbali, zikiwemo:

  • Uhasibu
  • Usimamizi wa Biashara
  • Uhandisi (Ujenzi, Umeme, Mitambo, Mafuta na Gesi)
  • Sayansi ya Kompyuta / TEHAMA
  • Uchumi na Mipango
  • Sheria
  • Lishe na Sayansi ya Chakula
  • Usimamizi wa Rasilimali Watu
  • Ununuzi na Ugavi
  • Takwimu

Na fani nyingine zilizoainishwa kwenye tangazo

Waombaji wanapaswa kuwa na ufaulu wa kuanzia daraja la pili la chini (Lower Second Class), huku waliosajiliwa na bodi za kitaaluma wakipewa kipaumbele.

Aidha, mwombaji hatakiwi kuzidi umri wa miaka 29 ifikapo Mei 2026.

Sifa za Mchunguzi Msaidizi (Nafasi 250)

Kwa upande wa Mchunguzi Msaidizi, waombaji wanatakiwa kuwa na cheti au astashahada katika fani za kiufundi au usaidizi, zikiwemo:

  • Ulinzi (Security Skills)
  • Ufundi wa magari (ikiwemo panel beating na upakaji rangi)
  • Udereva (leseni halali daraja C)
  • Huduma kwa wateja / Msaidizi wa ofisi
  • Uhasibu (Diploma)
  • Ukatibu muhtasi
  • Ufundi wa kompyuta
  • Matengenezo ya mashine za ofisi

Kwa mujibu wa tangazo, waombaji wa nafasi hizi wanapaswa kuwa raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 25.

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

TAKUKURU imeweka masharti ya jumla yanayopaswa kuzingatiwa na waombaji wote, yakiwemo:

  • Kuwa na uadilifu wa hali ya juu
  • Kutokuwa na rekodi ya uhalifu
  • Kuwa tayari kufanya kazi katika wilaya yoyote Tanzania Bara
  • Kutowahi kufukuzwa au kuachishwa kazi katika utumishi wa umma

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha nyaraka muhimu zikiwemo vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa, wasifu binafsi (CV), pamoja na mawasiliano ya wadhamini watatu. Aidha, namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ni ya lazima.

TAKUKURU imeonya kuwa:

“Mwombaji atakayewasilisha vyeti vya kughushi au kutoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.”

Vyeti vya elimu kutoka nje ya nchi vinapaswa kuthibitishwa na mamlaka husika nchini kama TCU, NACTVET au NECTA.

Utaratibu wa Kutuma Maombi

Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo rasmi wa ajira wa TAKUKURU kwa njia ya mtandao:

👉 ajira.pccb.go.tz

Kwa mujibu wa tangazo, maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kwa mkono hayatapokelewa.

Barua za maombi zinapaswa kuelekezwa kwa:

  • Mkurugenzi Mkuu,
  • Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),
  • Mtaa wa Jamhuri,
  • S.L.P. 1291,
  • 1101 Dodoma

Mwisho wa Kutuma Maombi

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 03 Mei 2026.

Waombaji watakaokidhi vigezo na kupita hatua ya awali ya uchambuzi ndio watakaowasiliana kwa hatua zinazofuata za mchakato wa ajira.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal
  2. Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Machi 2026
  3. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2026
  4. Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Uhamiaji
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo