Opah Clement Ajiunga Na Henan Fc Ya Ligi Kuu Ya China
Mshambuliaji wa kimataifa wa tanzania, Opah Clement tukumbuke (23) amejiunga na timu ya henan wanxian mountain wfc inayoshiriki ligi kuu ya wanawake china akitokea beşiktaş ya uturuki.
Opah Clement, ambaye awali aliwahi kuchezea Simba Queens, ameonyesha uwezo mkubwa katika soka la wanawake.
Akiwa na Beşiktaş, alijizolea sifa nyingi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kulisakata kabumbu na kutia kamba nyavuni.
Kabla ya kujiunga na Beşiktaş, Opah alicheza kwa mafanikio makubwa katika klabu ya Kayseri Women ya Uturuki, ambapo katika msimu wa 2021/22 alifunga mabao matano katika mechi tano tu.
Katika msimu wa 2023/24 Turkcell Women’s Football League akiwa na Beşiktaş, Opah aling’ara zaidi kwa kufunga mabao 12 katika mechi 10. Ufanisi huu umemuwezesha kupata mkataba na timu ya Henan Wanxian Mountain WFC ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Wanawake China.
Kwa sasa, Henan Wanxian Mountain WFC inakabiliwa na changamoto kubwa katika ligi, ikiwa katika nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi 13 bila kushinda, wakipoteza mechi sita na kutoa sare saba. Timu hii imefunga mabao nane na kuruhusu mabao 21 kufungwa.
Opah Clement anatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa na kusaidia timu yake mpya kupanda kwenye msimamo wa ligi. Kwa kuzingatia rekodi yake ya ufungaji bora, matumaini ya mashabiki wa Henan Wanxian Mountain WFC yameongezeka.
Wanawake wa Tanzania Katika Soka la Kimataifa
Opah Clement sasa anaungana na kundi dogo la wanasoka wa kike wa Kitanzania wanaocheza nje ya Afrika.
Clara Luvanga, ambaye anachezea Al Nassr Women FC huko Saudi Arabia, na Aisha Masaka ambae amesajiliwa na klabu ya Brighton Women FC huko England ni miongoni mwa wachezaji hawa.
Katika habari nyengine za uamisho, Simba Queens, mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) 2023/2024, wametangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Nigeria, Precious Christopher. Precious alikuwa mchezaji wa zamani wa Yanga Princess na Rivers Angels FC ya Nigeria.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Novatus Miroshi Ajiunga na Goztepe ya Uturuki
- Rasmi: Khomeini Abubakar Ajiunga na Yanga Akitokea Singida Black Star
- Yanga Yapata Mserereko CAF: Mechi Zote za Klabu Bingwa Kupigwa Dar es Salaam
- Tuzo ya Mchezaji Bora Ligi Kuu NBC 2023/2024: Hawa Ndio Wagombea
- Matokeo TS Galaxy Vs Yanga Leo 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki
Weka Komenti