Ratiba ya Azam FC Ligi Kuu 2024/2024 | Ratiba ya Mechi za Azam Fc Ligi Kuu ya NBC 2024/25
Azam Football Club, almaharufu kama “Wana Lambalamba” au “Matajiri wa Chamazi,” ni miongoni mwa vilabu vikubwa zaidi vya soka nchini Tanzania, vyenye historia iliyojaa mafanikio katika michuano mbalimbali ya soka la ndani na kimataifa.
Klabu hii yenye makazi yake Chamazi, Temeke jijini Dar es Salaam, inajiandaa kushiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania msimu wa 2024/2025, ikiwa na lengo la kuongeza taji jingine kwenye maktaba yao ya mafanikio.
Historia na Mafanikio ya Azam FC
Azam FC ilianzishwa mwaka 2004 ikiwa inajulikana kama Mzizima Football Club kabla ya kubadili jina mara mbili—Azam Sports Club mwaka 2005, na hatimaye Azam Football Club mwaka 2006. Mwaka 2010, klabu hii ilihamia rasmi kwenye uwanja wao wa kisasa, Azam Complex Chamazi, ambao umechangia sana kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya klabu hii.
Tangu kuanzishwa kwake, Azam FC imefanikiwa kujikusanyia mataji 10, ikiwa ni pamoja na:
- Taji 1 la Ligi Kuu ya Tanzania (2013/2014) waliloshinda bila kupoteza mechi yoyote.
- Kombe la Mapinduzi mara 5, rekodi ya kuwa klabu yenye ushindi mwingi wa kombe hilo.
- Kombe la Kagame mara 2, ikiwa ni klabu ya kwanza nchini kushinda kombe hilo bila kufungwa goli hata moja.
- Kombe la Shirikisho la Tanzania mara 1.
- Ngao ya Jamii mara 1.
Azam FC pia inajivunia kuwa na mashabiki wengi na washindani wakuu kama Yanga SC, Simba SC, Mtibwa Sugar FC, na Singida Fountain Gate. Ushindani huu unaleta mvuto mkubwa kwenye mechi za Ligi Kuu, hasa kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania.
Kwa msimu wa 2024/2025, Azam FC inatarajia kufanya vyema zaidi, wakilenga kushinda taji la Ligi Kuu na mashindano mengine ya ndani na nje ya nchi. Kikosi cha Azam FC kimeimarishwa kwa usajili wa wachezaji wapya wenye vipaji, na benchi la ufundi likiongozwa na kocha mzoefu, linajiandaa kukabiliana na changamoto za msimu mpya.
Ratiba ya Azam FC Ligi Kuu 2024/2024
Agosti 2024
- 28/08/2024 – JKT Tanzania (0 – 0) Azam Fc
Septemba 2024
- 26/09/2024 – KMC (16 : 00) Azam
- 29/09/2024 – Mashujaa (16 : 15) Azam
Oktoba 2024
- 03/10/2024 – Namungo (21 : 00) Azam
- 18/10/2024 – Tanzania Prisons (16 : 00) Azam
- 29/10/2024 – Azam (19 : 00) KenGold
Novemba 2024
- 03/11/2024 – Azam (19 : 00) Singida Black Stars
- 10/11/2024 – Young Africans PSTP Azam
- 23/11/2024 – Azam (19 : 00) Kagera Sugar
- 30/11/2024 – Dodoma Jiji (19 : 00) Azam
Desemba 2024
- 13/12/2024 – Tabora United (16 : 15) Azam
- 17/12/2024 – Azam (19 : 00) Fountain Gate
- 21/12/2024 – Azam (19 : 00) JKT Tanzania
- 28/12/2024 – Azam (21 : 00) KMC
Januari 2025
- 21/01/2025 – Pamba Jiji (16 : 00) Azam
- 26/01/2025 – Azam (19 : 00) Mashujaa
- 31/01/2025 – Coastal Union (19 : 00) Azam
Februari 2025
- 15/02/2025 – Simba (19 : 00) Azam
- 22/02/2025 – Azam (19 : 00) Namungo
Machi 2025
- 02/03/2025 – Azam (21 : 00) Tanzania Prisons
- 08/03/2025 – KenGold (16 : 15) Azam
- 30/03/2025 – Singida Black Stars (15 : 15) Azam
Aprili 2025
- 12/04/2025 – Azam (18 : 30) Young Africans
- 20/04/2025 – Kagera Sugar (PSTP) Azam
Mei 2025
- 02/05/2025 – Azam (21 : 00) Dodoma Jiji
- 17/05/2025 – Azam (16 : 00) Tabora United
- 24/05/2025 – Fountain Gate (16 : 00) Azam
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba YA Ligi Kuu Ya Zanzibar (Pbz Premier League) 2024/2025
- Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
- Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
- Ratiba Ya Ligi Kuu England 2024/2025 EPL
- Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu NBC 2024/2025
- Ratiba ya Simba Sc Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
- Mayele Akitabiria Mafanikio Makubwa Kikosi cha Yanga Msimu Huu
Weka Komenti