Ratiba ya Fainali Kombe La Shirikisho Afrika CAF 2024/2025

Ratiba ya Fainali Kombe La Shirikisho Afrika CAF 2024 2025

Ratiba ya Fainali Kombe La Shirikisho Afrika CAF 2024/2025

Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) mwaka 2025 itawakutanisha Simba SC kutoka Tanzania dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Mechi ya kwanza itapigwa tarehe 17 Mei 2025 katika Uwanja wa Berkane Municipal, Morocco, huku mechi ya marudiano ikichezwa tarehe 25 Mei 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mashabiki wa soka barani Afrika wanatarajia mtanange wa kusisimua baina ya vigogo hawa wawili walioweka historia kwenye mashindano ya klabu Afrika.

Ratiba Rasmi ya Fainali Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, ratiba ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ni kama ifuatavyo:

Mechi ya Kwanza (Mzunguko wa Kwanza):

  • Tarehe: 17 Mei 2025
  • Uwanja: Berkane Municipal, Berkane – Morocco
  • Timu: RS Berkane vs Simba SC

Mechi ya Marudiano (Mzunguko wa Pili):

  • Tarehe: 25 Mei 2025
  • Uwanja: Benjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam – Tanzania
  • Timu: Simba SC vs RS Berkane

Ratiba ya Fainali Kombe La Shirikisho Afrika CAF 2024/2025

Safari ya Simba SC Kufika Fainali

Simba SC imeandika historia mpya kwa kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kufika mara nyingi zaidi katika hatua ya fainali ya mashindano ya klabu Afrika. Timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, jijini Dar es Salaam, ilifuzu kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa jumla dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini. Simba ilishinda kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza nyumbani na kulazimisha sare ugenini, Aprili 28, 2025, matokeo yaliyowaweka salama kuelekea fainali.

Rekodi hii inaifanya Simba kujiweka mbele zaidi katika historia ya soka la Tanzania, kwa kuwa mara ya pili kuifikia hatua ya fainali ya mashindano chini ya mwamvuli wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), mara ya kwanza ikiwa mwaka 1993 walipofuzu kucheza fainali ya Kombe la CAF. Aidha, katika historia ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba SC ni klabu ya pili kutoka Tanzania kufika fainali, baada ya Yanga SC kufanya hivyo msimu wa 2022/2023. Hali hii inaashiria maendeleo makubwa ya klabu za Tanzania katika ramani ya soka la kimataifa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba SC Yatinga Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Baada ya Sare na Stellenbosch
  2. Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025
  3. Kikosi cha Simba SC vs Stellenbosch Leo 27 April 2025
  4. Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025 Saa Ngapi?
  5. Mayele Aipeleka Pyramid Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF
  6. Al Ahly Yamtimua Kocha Marcel Koller Baada ya Kutolewa Klabu Bingwa Afrika
  7. Mtibwa Sugar Yarejea Ligi Kuu NBC 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo