Ratiba ya Mechi za CAF Leo 28/11/2025

Ratiba ya Mechi za CAF Leo 28/11/2025

Michuano ya CAF leo inaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali barani Afrika, huku timu kutoka ukanda wa Kusini, Kaskazini, Mashariki na Magharibi mwa bara zikisaka pointi muhimu katika hatua za makundi. Mashabiki wanatarajiwa kushuhudia michezo yenye ushindani mkubwa, wakati miamba ya soka ikipambana kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele.

LIGI YA MABINGWA AFRIKA – Ratiba ya Mechi za CAF Leo 28/11/2025

Kulingana na ratiba rasmi, jumla ya michezo minne itachezwa leo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika:

LIGI YA MABINGWA AFRIKA – Ratiba ya Mechi za CAF Leo 28/11/2025

19:00 – JS Kabylie (Alg) vs Young Africans (Tan)

Young Africans kutoka Tanzania wapo Algeria kwenye uwanja wa Hocine Ait Ahmed katika mchezo muhimu dhidi ya JS Kabylie.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, mechi hii itarushwa mubashara kupitia AzamSports1HD. Wananchi wanaingia uwanjani wakiwa na morali ya ushindi walioupata kwenye mchezo uliotangulia, hali inayowapa hamasa ya kuendelea kusaka pointi ugenini.

19:00 – Rivers United (Nga) vs Berkane (Sea)

Rivers United ya Nigeria itawakaribisha Berkane katika mchezo mwingine wa kundi, ambapo timu zote zinahitaji matokeo chanya ili kubaki kwenye ushindani wa hatua za mtoano.

22:00 – FAR Rabat (Sea) vs Al Ahly (Egy)

FAR Rabat wana kazi ngumu dhidi ya mabingwa wa kihistoria, Al Ahly kutoka Misri. Mchezo huu unatarajiwa kuwa miongoni mwa mechi zenye ushindani mkubwa kutokana na rekodi za klabu zote mbili katika michuano ya CAF.

22:00 – MC Alger (Alg) vs Mamelodi (Rsa)

MC Alger wanawakaribisha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika pambano la usiku wa leo. Timu zote mbili zimekuwa zikifanya vizuri katika mechi za hivi karibuni, hivyo matokeo yanaweza kubadilisha hali ya msimamo wa kundi lao.

KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA – Ratiba ya Mechi za CAF Leo 28/11/2025

16:00 – Zesco Utd (Zam) vs Al Masry (Egy)

Zesco United ya Zambia watakuwa wenyeji wa Al Masry katika mchezo wa mapema leo jioni, huku pande zote zikisaka mwanzo mzuri kwenye michezo ya makundi.

19:00 – Azam FC (Tan) vs Wydad (Sea)

Azam FC watakuwa uwanja wa New Amaan Complex kuwakaribisha Wydad Casablanca. Kwa mujibu wa taarifa za klabu, mchezo huu utaanza saa 1:00 usiku na kurushwa mubashara kupitia AzamSports2HD. Klabu ya Azam FC imewataka mashabiki kuujaza uwanja, ambapo mashabiki 1,000 wa kwanza watapata nafasi ya kuingia bure, huku viingilio vikiwa:

  • VIP: TZS 2,000
  • Mzunguko: TZS 1,000

22:00 – Safi (Sea) vs USM Alger (Alg)

Safi ya Morocco itakipiga dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa mwisho wa Kombe la Shirikisho kwa siku ya leo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. TFF Yatangaza Kuahirishwa kwa Tuzo za Msimu 2024/2025
  2. Timu Tatu za Tanzania Zashindwa Kung’ara Katika Michezo ya Kwanza ya Makundi CAF
  3. Msimamo wa Makundi Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
  4. Msimamo Kundi la Simba Klabu Bingwa 2025/2026
  5. Matokeo ya Simba vs Petro De Luanda leo 23/11/2025
  6. Wachezaji Wanaowania Tuzo za TFF 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo