Timu zilizopanda Daraja Ligi Kuu ya England EPL 2024/2025

Timu zilizopanda Daraja Ligi Kuu ya England EPL 2024/2025 | Timu zilizopanda Daraya Ligi Kuu Uingereza

Ligi Kuu ya England (EPL) msimu wa 2024/2025 unakaribia kuanza, na tayari joto la ushindani limeshaanza kuwaka. Msimu wa 2023/2024 ulikuwa wa kipekee, ukiwa na mbio za ubingwa zilizochukua sura mpya kabisa. Manchester City walitamba kwa mara nyingine tena, wakitwaa taji lao la nne mfululizo, huku Arsenal wakishuhudia ndoto zao za ubingwa zikiyeyuka dakika za lala salama.

Lakini EPL siyo tu kuhusu vinara wa mbio za ubingwa. Kumekuwa na shangwe na nderemo kwa timu zilizofanikiwa kupanda daraja, huku machozi na majonzi yakitawala kwa wale walioshuka daraja. Msimu huu mpya unaanza huku mashabiki wakijiuliza, je, kutakuwa na mabadiliko gani? Je, ni timu zipi zitashangaza, na zipi zitakumbana na changamoto?

Timu zilizopanda Daraja Ligi Kuu ya England EPL 2024/2025

Baada ya msimu wa kusisimua katika Ligi ya Daraja la Pili Uingereza (EFL Championship), vilabu vitatu vimepata tiketi ya kucheza ligi kuu ya Uingereza EPL msimu ujao wa 2024/2025. Zifuatazo ndiyo timu zilizopanda daraja ligi kuu ya England

1. Leicester City

Leister City: Timu zilizopanda Daraja Ligi Kuu ya England EPL 2024/2025

Wakiwa mabingwa wa EFL Championship, Leicester wanarejea EPL baada ya msimu mmoja tu daraja la pili. Mashabiki wa “The Foxes” hawatasahau haraka ushindi wao wa kihistoria wa EPL mnamo 2016, na wanatarajia kurudia mafanikio hayo msimu huu.

2. Ipswich Town

Ipswitch: Timu zilizopanda Daraja Ligi Kuu ya England EPL 2024/2025

Baada ya miaka 22 ya kusubiri, Ipswich wanarejea EPL kwa kishindo. Chini ya uongozi wa kocha chipukizi Kieran McKenna, Ipswich walimaliza nafasi ya pili katika EFL Championship, na kuonyesha soka la hali ya juu msimu mzima.

3. Southampton

“The Saints” hawakukata tamaa baada ya kushuka daraja msimu uliopita. Walionyesha ukomavu mkubwa kwa kushinda mechi ya mchujo dhidi ya Leeds United, hivyo kupata nafasi yao EPL.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Picha Za Parade ya Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24
  2. Matokeo na Ratiba ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026
  3. Timu zitakazo shiriki CECAFA kagame Cup 2024
  4. Timu Inayoongoza kwa Magoli Ligi Kuu Ya NBC 2023/2024
  5. Guardiola Ashinda Tuzo Ya Kocha Bora EPL 2023/2024
  6. Mauricio Pochettino aondoka Chelsea Baada ya Msimu Mmoja
  7. Hawa Ndio Viungo Wanaoweza Kurithi Mikoba Ya Toni Kroos
  8. Mabadiliko ya Uwanja: Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB Kuchezwa Zanzibar
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo