Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025

Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo, tarehe 21 Oktoba 2025, limetangaza rasmi ratiba ya Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) 2025, unaotarajiwa kufanyika kitaifa katika shule zote za msingi nchini kuanzia tarehe 22 hadi 23 Oktoba 2025.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Ally Mohamed, jumla ya wanafunzi 1,582,140 kutoka shule 20,517 za Tanzania Bara wanatarajiwa kushiriki katika upimaji huo. Kati yao, wavulana ni 764,290 (asilimia 48.31) na wasichana ni 817,850 (asilimia 51.69).

Mtihani huu unafanyika kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 (Toleo la 2023) na Mtaala ulioboreshwa, unaolenga kuinua ubora wa elimu ya msingi kwa kuwajengea wanafunzi uelewa mpana wa masomo ya msingi.

Masomo Yatakayofanyika Katika Mtihani wa Darasa la Nne 2025

Kwa mwaka huu wa 2025, wanafunzi watafanya mtihani katika masomo sita ya lazima pamoja na masomo matatu ya hiari kama ifuatavyo:

Masomo ya lazima

  1. Sayansi (Science)
  2. Hisabati (Mathematics)
  3. Jiografia na Mazingira, Sanaa na Michezo (Geography and Environment, Arts and Sports)
  4. Kiswahili
  5. English Language
  6. Historia ya Tanzania na Maadili

Masomo ya hiari (chaguo moja pekee)

  1. Lugha ya Kifaransa
  2. Lugha ya Kiarabu
  3. Lugha ya Kichina

Ratiba Kamili ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025

Jumatano, 22 Oktoba 2025

Muda Somo
2:00 – 3:30 Sayansi (Science)
3:30 – 4:30 Mapumziko
4:30 – 6:00 Hisabati (Mathematics)
6:00 – 8:00 Mapumziko
8:00 – 9:30 Jiografia na Mazingira, Sanaa na Michezo (Geography and Environment, Arts and Sports)

Alhamisi, 23 Oktoba 2025

Muda Somo
2:00 – 3:00 Kiswahili
3:00 – 4:00 Mapumziko
4:00 – 5:00 English Language
5:00 – 5:30 Mapumziko
5:30 – 6:30 Lugha za Kigeni (French / Arabic / Chinese)
6:30 – 8:00 Mapumziko
8:00 – 9:30 Historia ya Tanzania na Maadili

Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025

Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi na Wasimamizi

NECTA imetoa maelekezo muhimu kwa waalimu, wasimamizi na wanafunzi wote watakaoshiriki katika mtihani wa mwaka huu:

  • Hakikisha unayo ratiba rasmi ya upimaji wa mwaka 2025 kama ilivyotolewa na NECTA.
  • Soma jina la somo juu ya bahasha kabla ya kufungua karatasi za mtihani.
  • Mwanafunzi atasome kwa sauti jina la somo lililoandikwa juu ya bahasha ili kuthibitisha usahihi.
  • Endapo kutatokea utofauti kati ya ratiba na maelekezo ya karatasi ya mtihani, yale yaliyomo katika karatasi ndiyo yatakayofuata.
  • Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wataongezewa muda wa dakika 20 kwa kila saa kwenye somo la Hisabati na dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine.
  • Wanafunzi wenye uoni hafifu watapewa karatasi zenye maandishi makubwa yaliyotolewa na NECTA.
  • Wanafunzi wote waingie darasani nusu saa kabla ya mtihani kuanza, na watakaochelewa zaidi ya nusu saa hawataruhusiwa kuingia.
  • Wanafunzi wanapaswa kufuata maelekezo ya wasimamizi, kuandika majina yao kwa usahihi, na kuepuka udanganyifu wa aina yoyote.

Bofya Hapa Kupakua Ratiba Rasmi ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Mbeya
  2. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Dar es salaam
  3. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Arusha
  4. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Kilimanjaro
  5. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Iringa
  6. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Yatatangazwa Lini na NECTA?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo