Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC) 2024 | Walioitwa kwenye Usaili NEC: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Katiba hiyo, Ibara ya 65, inaelekeza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani ufanyike kila baada ya kipindi cha miaka mitano (5).
Tanzania inatumia mfumo wa uchaguzi ambao mgombea mwenye kura nyingi kuliko mgombea mwingine hutangazwa kuwa mshindi (First Past The Post). Hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 41 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, Kifungu cha 35F(8) na Kifungu cha 81 (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 82 (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi, Waandishi Wasaidizi, na ”BVR Kit Operators”. Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura pia wanashirikishwa.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 15A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Kifungu cha 17A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura. Mawakala hawa wanawajibika kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia sheria, kanuni, na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwaka 2024, NEC imeitisha usaili kwa ajili ya kujaza nafasi mbalimbali zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi. Katika makala hii, tumekuletea orodha ya walioitwa kwenye usaili pia tutajadili maandalizi ya usaili, na nini cha kufanya baada ya usaili.
Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC) 2024
Hapa chini tumekuletea viungo unavyoweza kutumia kudownload majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC) 2024 katika halmashauri mbalimbali. Kila kiungo kinahusiana na orodha ya majina ya waombaji wa ajira walioteuliwa kwa ajili ya usaili, ikijumuisha tarehe, muda, na mahali pa kufanyia usaili. Tafadhali bonyeza kiungo cha halmashauri yako ili kupata maelezo zaidi na kuhakikisha umejiandaa ipasavyo kwa hatua inayofuata katika mchakato wa ajira.
Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC) Nsimbo 2024
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Uchaguzi Nsimbo anawatangazia waombaji kazi nafasi za Mwandikishaji Msaidizi na Mwendesha BVR Kufika kwenye usaili. Vituo vya usaili na maelezo mengine yanapatikiana kwenye viunganishi vya kata hapa chini.
- Usaili Kata Ya Ibindi.Pdf
- Usaili Kata Ya Itenka.Pdf
- Usaili Kata Ya Kanoge.Pdf
- Usaili Kata Ya Kapalala.Pdf
- Usaili Kata Ya Katumba.Pdf
- Usaili Kata Ya Litapunga.Pdf
- Usaili Kata Ya Machimboni.Pdf
- Usaili Kata Ya Mtapenda.Pdf
- Usaili Kata Ya Nsimbo.Pdf
- Usaili Kata Ya Sitalike.Pdf
- Usaili Kata Ya Ugalla.Pdf
- Usaili Kata Ya Uruwira.Pdf
Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC) 2024
Walioitwa Kufanya Usaili Jimbo La Bukene-Nzega Dc.Pdf
Walioitwa Kufanya Usaili Jimbo La Nzega Vijijini-Nzega Dc.Pdf
Editor’s Picks:
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili jeshi la Polisi 2024
- Nafasi Mpya za Kazi Halmashauri ya Wilaya Mufindi (Mwisho wa Maombi ni 04/08/2024)
- Ajira Mpya za Walimu Tanzania 2024: Nafasi 11,015 Zatangazwa, Maombi Hadi Agosti 2
- Nafasi Mpya za Kazi Almashauri ya Wilaya ya Kibiti (Mwisho wa Maombi 28 Julai, 2024)
- Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Yatangaza Nafasi za Kazi (Mwisho 25/07/2024)
Weka Komenti