Ratiba ya Yanga Klabu Bingwa 2025/2026

Ratiba ya Yanga Klabu Bingwa 2025/2026

Baada ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya Young Africans SC inaanza safari ya kutafuta nafasi ya kufika hatua ya mtoano kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika msimu wa CAF Champions League 2025/2026. Timu hiyo imepangwa kwenye Kundi B, ikiwa na wapinzani wenye uzoefu katika mashindano ya kimataifa: Al Ahly (Misri), Kabylie (Algeria), na AS FAR (Morocco).

Hapa tumekuletea Ratiba ya Yanga Klabu Bingwa 2025/2026 kwa michezo yote ya hatua ya makundi kama ilivyopangwa na waandaaji wa mashindano. Ratiba inaonyesha tarehe za mechi, wapinzani, na muendelezo wa michezo kuanzia raundi ya kwanza hadi ya sita.

Ratiba ya Yanga Klabu Bingwa 2025/2026

Ratiba ya Mechi za Yanga Klabu Bingwa 2025/2026 Kundi B

📅 21/11/2025 – Saa 19:00

  • Young Africans 🆚 AS FAR

Katika mchezo wa kwanza, Young Africans inaanza kampeni nyumbani dhidi ya AS FAR. Huu ndio mchezo muhimu wa kufungua hesabu za pointi.

📅 28/11/2025 – Saa 19:00

  • Kabylie 🆚 Young Africans

Safari ya kwanza ya ugenini kwa Young Africans, wakikabiliana na Kabylie kutoka Algeria.

📅 23/01/2026 – Saa 19:00

  • Al Ahly 🆚 Young Africans

Mchezo wa tatu na wa kwanza wa mwaka 2026 unaikutanisha Young Africans na Al Ahly, mabingwa mara nyingi wa michuano hii.

📅 30/01/2026 – Saa 19:00

  • Young Africans 🆚 Al Ahly

Baada ya wiki moja, Young Africans watakuwa wenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa marudiano.

📅 06/02/2026 – Saa 19:00

  • AS FAR 🆚 Young Africans

Mchezo muhimu wa kukamilisha mechi za ugenini kwa Young Africans kwenye hatua hii ya makundi.

📅 13/02/2026 – Saa 19:00

  • Young Africans 🆚 Kabylie

Mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi utachezwa nyumbani, ukiamua nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi.

Muhtasari wa Ratiba Ya Yanga Club Bingwa 2025/2026 Hatua ya Makundi

Raundi Tarehe Mchezo Saa
1 21/11/2025 Young Africans vs AS FAR 19:00
2 28/11/2025 Kabylie vs Young Africans 19:00
3 23/01/2026 Al Ahly vs Young Africans 19:00
4 30/01/2026 Young Africans vs Al Ahly 19:00
5 06/02/2026 AS FAR vs Young Africans 19:00
6 13/02/2026 Young Africans vs Kabylie 19:00

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga vs KMC Leo 09/11/2025 Sasa Ngapi?
  2. Kikosi cha Simba vs JKT Tanzania Leo 08/11/2025
  3. Kikosi cha Yanga vs KMC Leo 09/11/2025
  4. Ratiba ya Ligi Kuu Wanawake Tanzania (TWPL) 2025/2026
  5. Droo ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
  6. Yanga Yaangukia Kundi B na Al Ahly Droo ya Makundi Klabu Bingwa 2025/2026
  7. Msimamo Kundi la Yanga Klabu Bingwa 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo