Serikali Yatoa Ufafanuzi Pamba Jiji Kufanya Mazoezi Gizani Uwanja wa Taifa

Serikali Yatoa Ufafanuzi Pamba Jiji Kufanya Mazoezi Gizani Uwanja wa Taifa

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa ufafanuzi rasmi kuhusiana na video zilizosambaa mitandaoni zikionesha wachezaji wa klabu ya Pamba Jiji FC wakifanya mazoezi gizani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa (maarufu kama Uwanja wa Taifa). Taarifa hiyo imebainisha kuwa tukio hilo lilitokea kutokana na timu ya Pamba Jiji kutowasilisha taarifa mapema kwamba wangehitaji kufanya mazoezi ya usiku kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Yanga SC uliopangwa Septemba 24, 2025.

Serikali Yatoa Ufafanuzi Pamba Jiji Kufanya Mazoezi Gizani Uwanja wa Taifa

Chanzo Cha Pamba Kufanya Mazoezi Gizani

 

View this post on Instagram

 

A post shared by DMTV (@dmtv5152)

Kwa mujibu wa Wizara, kikosi cha Pamba Jiji kilifika kwenye Uwanja wa Taifa majira ya saa 12:35 jioni bila kutoa taarifa ya mapema. Kufuatia hali hiyo, wataalamu wa umeme ambao kwa kawaida huhakikisha uwanja unakuwa na mwanga wa kutosha walikuwa tayari wameondoka. Baada ya hali hiyo kuonekana, menejimenti ya uwanja ililazimika kuwaita wataalamu hao tena kazini ili kuwasha taa, na mwanga wa uwanja uliwashwa rasmi majira ya saa 1:08 usiku.

Katika taarifa yake, Serikali imesema imesikitishwa na kusambaa kwa picha mjongeo za mazoezi hayo gizani, kwa kuwa chanzo cha hali hiyo ni makosa ya timu ya Pamba Jiji FC yenyewe.

Wizara imeeleza kuwa kitendo cha kusambaza video hizo kimeonekana kama jaribio la kuharibu heshima na taswira ya menejimenti ya uwanja, ambao mara zote umekuwa ukisimamiwa kwa kuzingatia taratibu na kanuni zilizowekwa.

Aidha, Wizara imetoa wito na onyo kwa timu zote zinazotumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kuhakikisha zinazingatia taratibu zilizopo. Timu zinapaswa kutoa taarifa mapema endapo zitahitaji kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya michezo yao, ili maandalizi yote muhimu ikiwemo huduma za umeme na usalama viweze kufanyika kwa wakati.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 Saa Ngapi?
  2. Ratiba ya Mechi za Leo 24/09/2025
  3. Fadlu Davids Atambulishwa Kama Kocha Mkuu wa Raja Casablanca ya Morocco
  4. Lamine Yamal Abeba Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka (Kopa Trophy)
  5. Simba Yamtambulisha Hemed Suleiman Kama Kocha wa Mpito
  6. Ousmane Dembélé Ashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2025
  7. Viwango Vya FIFA Duniani 2025 (FIFA Rankings)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo